Breaking News

Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Yakutana na Waandishi Wa Habari

Na Hellen Mtereko, Mwanza

Ofisi ya Taifa ya ukaguzi imekutana na waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuwajengea uwezo juu ya kuandika,kuripoti habari zao.

Ofisi hiyo imefanya kikao kazi na waandishi kutoka Kanda ya ziwa febuari 2,2021 katika ukumbi wa Halimashauri ya Jiji la Mwanza.

Akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho msaidizi wa Mkaguzi Mkuu wa hesabu za  Serikali Kanda ya ziwa, Anna Masanja amesema  lengo la kikao hicho ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari juu ya utoaji wa taarifa za viashiria vya rushwa.


Msaidizi wa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Kanda ya ziwa Anna Masanja akifungua kikao kazi kilichohusisha  Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na waandishi wa habari .

No comments