INTERNEWS NA MPC WAADHIMISHA SIKU YA RADIO DUNIANI MKOANI MWANZA.
Na Blandina Aristides
Mwanza.
Shirika la Intetnews Kwa kushirikiana na Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza (MPC) limeadhimisha siku ya Radio duniani jijini Mwanza kwa kutoa semina elekezezi kwa Baadhi ya waandishi wa habari na watangazaji wa Radio Mkoani hapa.
Semina hiyo ililenga kuwajengea uwezo waandishi na watangazaji wa Radio kuhusu namna Bora ya kusimamia maadilili yao Katika kutekeleza majukumu ya Kazi ikiwa ni pamoja na matumizi ya Lugha sahihi Katika utangazaji.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel, amefungua semina hiyo Kwa kuwataka waandishi na watangazaji wa Radio kutumia nafasi hiyo Kwa kuibua mambo yenye kuchochea maendeleo ya Mkoa Kwa kua wao ndio wenye jicho Kubwa la kuonesha mambo hayo.
Pia amewataka kufuata maadili ya Kazi kwani radio ikitumika vibaya inaweza kuingiza nchi kwenye machafuko yasiyotarajiwa.
Ameeleza kuwa kama ilivyo Kwa nchi zilizo endelea, Tanzania nayo ni miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki inayokua Kwa Kasi kwenye mawasiliani ikiwemo radio hivyo ipo haja ya kuhakikisha weredi Katika utangazaji unaimarika.
"Katika ukuaji wa mawasiliano ya tasnia ya ukuaji wa habari, radio imekua ikiaminiwa Zaidi Katika utoaji wa habari ikifuatiwa na magazeti na runinga" alisema Mhandisi Gabriel.
Shabani Mganga ni Mratibu wa Shirika Hilo ambaye ameeleza kuwa internews imekua na Miradi mbalimbali yenye lengo la kujengea uwezo vyombo vya habari nchini Ili viweze kufanya Kazi Kwa weledi Zaidi na maarifa.
" Ili waandishi wafanye Kazi zenye ubora na zinazo stahiki sisi kama internews ni jukumu letu kuwajengea uwezo na kuwafundisha namna Bora ya utangazaji ikiwa ni pamoja na matumizi sahihi ya Lugha ya Kiswahili" .Alisema Shabani.
Akizungumza Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza Edwin Soko, Mjumbe wa Klabu hiyo Tonny Alphonce ameeleza kuwa, Mkoa wa Mwanza unazo fursa mbalimbali hivyo ni vema waandishi na watangazaji wakatumia vyombo vyao kuzitangaza fursa kwa ufasaha.
Alisema watangazaji wa Radio, wananafasi Kubwa ya kuwa wabunifu Katika utengenezaji wa vipi maalumu vikiwemo vya maendeleo lakini pia vipindi vya kuadhimisha siku hii muhimu Kwa watangazaji wote nchini
Siku ya Radio duniani huadhimishwa Kila ifikapo February 13 Kila mwaka hivyo radio zitumie maadhimisho haya kujifunza namna Bora ya kutangaza kupitia watangazaji mahili na wabobezi Katika kukuza tasnia hii upande wa utangazaji.
Mwisho.
Play Casinos Near Washington, DC - MapYRO
ReplyDeleteFind the best casinos near Washington, DC 대전광역 출장안마 with 인천광역 출장샵 detailed reviews, photos and maps.What are the best casinos near 경상북도 출장마사지 Washington, DC?How 성남 출장마사지 long does it 포항 출장샵 take to find a good casino?