Breaking News

EMEDO NA TAWFA WAJA NA MPANGO WA KUPAMBANA NA CHANGAMOTO ZA WANAWAKE WAVUVI WA KANDA YA ZIWA.

     Na Tonny Alphonce,Mwanza

Shirika la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo (EMEDO) kwa kushirikiana na shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) pamoja Wizara ya Mifugo na Uvuvi wanakuja na mradi wa kuimarisha Umoja wa Wanawake Wanaojihusisha na Shughuli za Uvuvi Tanzania (TAWFA).

Bi Editrudith Lukanga mkurugenzi wa Shirika la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo (EMEDO) akizungumza na viongozi wa TAWFA

Akizungumzia mradi huo Bi Editrudith Lukanga amesema kwa kuanza mradi huo utawawezesha TAWFA kuchagua viongozi wake kuanzia ngazi ya Wilaya hadi Mkoa.

Ameongeza kuwa shirika la EMEDO kwa upande wake litahakikisha TAWFA inajiimarisha katika Ukanda huu wa Ziwa ili ianze kuwa na wajumbe wake kuanzia ngazi ya wilaya,Mkoa na hatimaye ishiriki vema katika ngazi ya Taifa.

Lucy Kilanga Afisa Masuala ya Kijinsia EMEDO akiwaelezea  viongozi wa TAWFA namna  mradi utakavyo wawezesha kujisimamia wao wenyewe.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi huo Lucy Kilanga amesema kwa kuanza EMEDO kwa kushirikiana na FAO wameanza kuwajengea uwezo viongozi wa mpito wa TAWFA ili waweze kwenda kusimamia vema mchakato wa kuwapata viongozi wake pamoja na kuanza kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili Wavuvi wanawake.

‘Tunaamini kupitia mradi huu viongozi hawa wakitoka hapa wanaweza kutatua changamoto mbalimbali zikiwemo zile za masoko na kwa muda huu wa miezi saba tutaendelea kuwasimamia TAWFA na baada ya hapo tunaamini kabisa watakuwa wameimarika na wataweza kwenda wenyewe.alisema Lucy’

Beatrice Mbaga mwenyekiti wa TAWFA Taifa amesema anaamini sasa umoja huu utakuwa na tija kwa kuwa sasa unashuka chini kwa kupata viongozi ambao wapo karibu zaidi na wavuvi.



'Kupitia mfumo huu wa uongozi naamini kabisa wamama hawa sasa wataongea lugha moja kwa kuwa watakuwa na viongozi wanaotoka katika maeneo yao hivyo ni rahisi kushirikiana katika mambo mbalimbali.alisema Beatrice'

PICHA ZAIDI











No comments