Breaking News

Wananchi Kanda ya ziwa washauriwa kuacha kutunza fedha kwenye vibubu.


Kaimu Meneja wa bank ya CRDB Japhary Hassanaly akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake

Na Hellen Mtereko, Mwanza

Wananchi Kanda ya ziwa wameshauriwa kuacha kutumia vibubu kwaajili ya kutunza fedha badala yake watumie taasisi za kifedha  kwaajili ya usalama wa fedha zao.

Ushauri huo umetolewa na Kaimu Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Japhary Hassanaly wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Amesema kunafaida kubwa sana kufanya shughuli mbalimbali na taasisi za kifedha ikiwemo fedha kuwa salama sanjari na kupata faida kutokana  na kile ambacho unakuwa umekihifadhi, ukilinganisha na kibubu ambacho kinaweza kuibiwa.

Hassanaly amesema kuwa wanaendelea kuboresha huduma kwa wateja zaidi na zaidi ili hamasa iwe kubwa kwa wananchi kuendelea kuitumia Benki hiyo.

Mwishoooo

No comments