WAJAWAZITO WATAKIWA KUANZA KLINIKI MAPEMA KUEPUSHA VIFO
Na Tonny Alphonce,Mwanza
Wajawazito wametakiwa kuanza kliniki mara moja pindi wanapobaini kuwa ni wajawazito kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kukabiliana na ongezeko la watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.
Ushauri huo umetolewa na afisa maendeleo na ustawi wa jamiii wa chama cha wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi Thelesia Jacob katika hafla iliyoandaliwa na aliyekuwa Miss Mwanza mwaka 2013 Lucy Charles yenye lengo la kushiriki chakula cha pamoja na watu wenye umelavu ili kusikilia changamoto zinazowakabili.Akizungumza katika
hafla hiyo Thelesia amesema kuna baadhi ya wajawazito hawazingatii taratibu na
miongozo ya kuhudhuria kiliniki jambo linalosababisha madhara ikiwemo ya Watoto
kuzaliwa wakiwa na tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi.
‘Mama anapochelewa
kuanza kliniki mapema anaweza kupata matatizo mbalimbali ya kiafya kwa upande
wake na kwa mtoto na ndio maana wataalamu wa afya wanasisitiza mama aanze
kuhudhuria kliniki mara baada ya kujigundua kuwa na ujauzito.alisema’
Kwa upande wake liyekuwa Miss Mwanza mwaka 2013 Lucy Charles amesema watu wenye ulemavu wanakabiliwa na changamoto nyingi hivyo kupitia taasisi yake ya Tabasam na Lucy Charles anakusudia kuwashika mkono ili na wao waweze kufikia ndoto zao.
‘Huu ni
mwendelezo wa kazi zinazofanywa na taasisi yangu ikiwa ni sehemu ya kurudisha
kile tunachokipata kwenye jamii na kuwa kuwarudishia tabasamu wale waliolipoteza
kutokana na matatizo mbalimbali.alisema Lucy’
Kwasasa
Mwanamitindo huyo pia ni muigizaji wa filamu na amesema kupitia jukwaa hilo
anakusudia kuinua vipaji kupitita Sanaa ya maigizo.
Miongoni mwa
watu wenye walemavu walioshiriki kwenye hafla hiyo Zainab Habibu na Habibu
Mrope wameomba watu binafsi na mashirika mbalimbali kujitokeza kuwasaidia
kwasababu bado wanakabiliwa na changamoto lukuki.
No comments