Breaking News

Viongozi wa dini washauriwa kutoa fedha zao kusaidiwa wenye uhitaji.


Askofu Mkuu wa Kanisa la The Sowers Evangelistic International Church Daniel Kulola akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake


Na Hellen Mtereko, Mwanza

Viongozi wa dini wameshauriwa kujitoa zaidi katika kunisaidia jamii hususani kwa wale watu wenye mahitaji maalum na wasiyojiweza ili na wao wajione ni sehemu ya jamii.

Rai hiyo imetolewa na Askofu mkuu wa kanisani la The Sowers Evangelistic  International Church (SEIC)  Dkt. Daniel Kulola alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mkoani Mwanza.

Dkt.Kulola amesema kuwa ni vema kuwekeza kwa jamii ili hata wanapokuwa katika nyumba za ibada inakuwa ni rahisi kusikiliza kile kinachokuwa kikifundishwa kutoka kwa kiongozi wa imani.

"Mimi nimejipanga katika miezi 12 ijayo na nina tos wito kwa Wananchi tusiusemee vibaya mwezi Januari kikubwa ni kujipanga na tujijengee tabia ya kuweka muda wa maombi na ndivyo dini zinavyotuelekeza na tuitumie vema fedha zetu kwa kuisaidia jamii ili kusudio la Mungu liweze kutuona na siyo kukimbilia starehe"alisema Kulola.

Ametoa rai pia kwa jamii kujiweka karibu na Mungu ilikuweza kuepuka majanga ambayo yanaweza kuliangamiza jamii na kujiandaa kuupokea mwaka mpya wa 2022 kimwili ,kiroho na kiuchumi ili kuendelea kujipanga zaidi katika maendeleo.

Mwishooo

No comments