MKURUGENZI WA HOLY LAND PRE AND PRIMARY SCHOOL AWAPANDISHA NDEGE WANAFUNZI WAKE WALIOFAULU MTIHANI WA TAIFA.
Na Tonny Alphonce,Mbeya
Mkurugenzi wa shule ya Holy
Land Pre and Primary School iliyoko Chunya Mkoani Mbeya,Lawena Nsonda
ametimiza ahadi yake ya kuwapeleka jijini Dr es Salaam wanafunzi wote wa darasa la nne waliofaulu
katika mtihani wao wa Taifa.
Mkurugenzi wa shule ya Holy Land Pre and Primary Bwana Lawena Nsonda (Baba Mzazi) wa pili kulia akiwa na Wanafunzi 7 walioongoza kitaifa katika mtihani wa Darasa la Nne wakiwa tayari kuelekea jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Lawena Nsonda amesema alitoa ahadi hiyo
mwaka jana wakati wanafunzi hao wakijiandaa na mitihani ya Taifa ikiwa njia
moja wapo ya kuwapa motisha ya kufanya vizuri katika mtihani huo.
Wanafunzi hao 7 ambao wote mwaka huu wanaingia darasa
la tano walisafiri na Ndege ya Air Tanzania kutoka mkoani Mbeya kwenda jijini
Dar es Salaam na kutembelea maeneo mbalimbli ya jiji hilo.
Mkurugenzi Lawena amewapongeza wanafunzi hao wa Holy
Land Pre and Primary School kwa kupata matokeo mazuri na kusisitiza kuendelea
kuwekeza zaidi katika walimu wazuri ili kupata matokeo mazuri zaidi kwa kila
mwaka.
“Nimeanza na hawa kutimiza ahadi niliyotoa
walikuwa na ndoto ya kupanda Ndege na kufika Jijini Dar es Salaam na nimefanya
hivyo,sasa na mwaka huu nitatoa ahadi kubwa zaidi ya hii ya mwaka jana.alisema
Mkurugenzi Lawena”
Holy Land Pre and Primary School iliyopo katika kundi
la watahiniwa pungufu ya 40 imeshika nafasi ya kwanza kitaifa kati ya shule
3997 matokeo ya darasa la nne yaliyotangazwa hivi karibuni.
No comments