Breaking News

Bilioni 1.5 zatolewa na Halimashauri ya Jiji la Mwanza kwaajili ya ujenzi wa madarasa


Vyumba vya madarasa vilivyokabidhiwa

Na Hellen Mtereko, Mwanza

Wilaya ya Nyamagana imekabidhi vyumba vya madarasa 39  vilivyojengwa kwa fedha za  uviko 19 ili kupunguza changamoto ya ukosefu wa madarasa kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na masomo mwaka 2022.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kabla ya kukabidhi madarasa hayo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Sekiete Seleman alisema kuwa Halmashauri imetoa billion 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa kwa mfumo wa maghorofa ili kuendelea kuwa na matumizi mazuri ya ardhi.

Muonekano wa vyumba vya madarasa vinavyo endelea kujengwa kwa mfumo wa gorofa.

Amesema elimu bora inatokana na miundombinu mizuri itakayomuwezesha mwanafunzi kusoma bila shida ndio maana tunajitahidi kuongeza madarasa ili kila Mtoto apate kusoma bila shida.

Amesema kuwa wazazi wafanye maandalizi ya kutosha kwaajili ya watoto ili wanapoanza masomo wasiwe na upungufu wa mahitaji yanayohusu shule.

Mwishooo

No comments