Zaidi ya milioni mbili kushindaniwa katika mbio za mitumbi zitakazo fanyika Jijini Mwanza
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Kampuni ya The Scope solutions imeandaa mashindano ya mitumbwi ya Tanzania Boat Race ambayo yatafanyika Desemba 4,2021 katika kisiwa cha ukerewemonanchi huku kilele cha mashindano hayo kufanyika Desemba 12,2021 Mkoani Mwanza mwaloni katika soko la samaki.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo msimu wa mwaka wa 202, Meneja Kanda ya ziwa kutoka kampuni ya The Scope solutions Ayubu Sossy amesema kuwa mashindano yanatarajiwa kujumuisha zaidi ya timu 60 za Wavuvi Mkoani hapa na Mikoa iliyopo kwenye ukanda wa ziwa Victoria.
Amesema kuwa mashindano hayo yanalenga kukuza utalii,kutangaza utamaduni wa kitanzania sanjari na uhamasishaji wa Jamii kujikinga na maambukizi ya magonjwa hatarishi kama, Malaria, VVU na UKIMWI, hususani kwa Vijana ambao ndio washiriki wengi pamoja na kutoa hamasa juu ya chanjo ya UVIKO 19.
Kwa upande wake Meneja wa TBL Mwanza Issa Makani ambao ni miongoni mwa wadhamini wa mashindano amesema kuwa kuna umuhimu wa kuendelea kushirikiana na waandaji wa mashindano hayo kutokana na fursa ya kuwakutanisha Watanzania pamoja ili waweze kuendelea kujifunza na kufikia malengo pamoja na kupata elimu kutoka kwa wataalamu wa afya ambao watatoa nafasi ya kupima magonjwa mbalimbali.
Mwishoooo
No comments