WADAU WANAOTOA HUDUMA ZA WATOTO WATAKIWA KUWAKUMBUKA WATOTO WALIOKO PEMBEZONI
Na Tonny Alphonce,Dodoma.
Serikali imewataka wadau wanaotoa huduma za watoto nchini kuangalia pia namna ya kutoa huduma hizo kwa watoto waliopo pembezoni ili nao waweze kupata huduma muhimu kama ilivyo kwa watoto wanaopatikana katika miji mikubwa.
Kauli hiyo imetolewa na yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mh
Mwanaidi Ally Khamisi wakati wa ufunguzi wa mafunzo
maalumu kwa waandishi wa habari za watoto 26 uliofanyika mkoani Dodoma
ikiwa ni maandalizi ya kuanza kwa mradi mpya uliopewa jina la mtoto kwanza.
Amesema kukosekana
kwa wadau wanatoa huduma za Malezi,Makuzi na Maendeleo
ya awali ya mtoto katika maeneo ya vijijini inasababisha kukosekana kwa
uwiano sawa na kusababisha makuzi yasiyo timilifu kwa watoto.
Naibu
Waziri amewataka wadau wote wa Watoto kuwasiliana kabla ya kuanza kutoa huduma
ili kujua ni maeneo gani yanye uhitaji mkubwa na nguvu zielekezwe huko ili
kuhakikisha Watoto wote wa Tanzania wanapata huduma muhimu ya Malezi na Makuzi
kwa usawa.
Akizungumzia
baadhi ya hatua ambazo serikali imechukua katika kuboresha huduma za Malezi,Makuzi
na maendeleo ya awali ya mtoto Naibu Waziri amesema tayari serikali imeandaa
miongozo na sera mbalimbali ikiwa ni pamoja na sera ya maendeleo ya mtoto ya mwaka
2008,kutunga sheria ya mtoto no 21 ya mwaka 2009,sheria ya elimu yam waka 1978
pamoja na serikali kuwashirikisha wadau kutekeleza mpango wa Taifa wa
kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na Watoto kwa kipindi cha mwaka 2017/2018
hadi 2021/2022.
Wanahabari Vinara wa Habari za Watoto wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri Mh Mwanaidi hayupo pichani.
Akizungumzia kuwepo kwa wanahabari bingwa wa habari za watoto,Naibu Waziri Mh Mwanaidi amewataka wanahabari hao kuendelea kuihabarisha jamii kuhusu umuhimu wa Malezi na Makuzi kwa mtoto kwa kuwa bado wananchi wengi hawana ufahamu wa huduma za Malezi na Makuzi ya awali ya mtoto.Awali akitoa
salamu za UTPC katika ufunguzi huo wa mafunzo maalumu kwa waandishi wa habari
za Watoto mkurugenzi wa UTPC,Abubakari Karsan amewapongeza vinara hao kwa
kuandika Habari zaidi ya 1000 ndani ya miaka mitatu.
Karsani
amesema jambo hilo si dogo na linapaswa kupongezwa kwa kuwa tangu kuanza
kuandikwa kwa habari za watoto kumesaidia kuleta matokeo chanya katika baadhi
ya maeneo hapa nchini.
‘Mgeni
rasimi nataka niseme tu yawezekana jambo hili likaonekana la kawaida lakini si
la kawaida waandishi hawa wanastahili pongeze na wamefanyakazi kubwa sana
katika kuandika habari hizi za watoto’,alisema Karsan.
Mkurugenzi Karsani
amewataka pia wadau wengi ambao wanahitaji waandishi wenye uwezo mkubwa kama
ilivyo kwa vinara hao wa ECD kuwasiliana na uongozi wa UTPC ili waweze
kufanikiwa katika jambo ambalo wamekusudia kulifikisha katika jamii.
No comments