Breaking News

Waajiri waombwa kupima afya za wafanyakazi wao wa nyumbani kabla ya kuwapa mikataba



Na Hellen Mtereko, Mwanza

Waajiri wameombwa kuweka utaratibu wa kuwapima afya wafanyakazi wa nyumbani kabla ya kuwapa mikataba ili waweze kujua afya zao hali itakayosaidia kupunguza maambukizi mapya katika familia.

Ombi hilo limetolewa leo na Afisa ustawi wa Jamii kutoka Shirika la kutetea haki za Watoto wafanyakazi wa Nyumbani (WOTESAWA) Renalda Mambo ikiwa ni siku ya ukimwi duniani inayoadhimishwa Desemba 1 kila mwaka ambapo kwa mwaka huu imebeba kauli mbiu isemayo "zingatia usawa.tokomeza UKIMWI,tokomeza Magonjwa ya mlipuko",

Mambo amesema kuwa waajiri wengi wanawachukua wafanyakazi wa nyumbani bila kujua afya zao na hivyo kusababisha madhara kwa famila hivyo ni vema wafahamu afya zao ili kuweza kuwasaidia pia katika kuwapatia matibabu.

Amesema kuwa wotesawa wamekuwa wakitoa elimu kwa Watoto hao wanaofanya kazi za nyumbani juu ya umuhimu wa kujua afya zao,madhara ya mimba za utotoni, jinsi ya kuishi kwa waajiri wao sanjari na kuelewa umuhimu wa mkataba wa kazi.

Amesema kuwa Jamii iishi vizuri na wafanyakazi wa nyumbani ili kuweza kupunguza au kumaliza kabisa vitendo vya ukatili kwani mfanyakazi wa nyumbani akiwa salama familia pia itakuwa salama.

Mwishooo

No comments