TAASISI ZA DINI ZAITAKA SERIKALI KUZILIPIA KAYA MASIKINI BIMA.
TAASISI za dini mbalimbali hapa nchini zinazounda jumuiya ya kikiristo,Bakwata, na baraza la maaskofu katoliki wameiomba Serikali kuweka mfumo wa kuwalipia Bima ya Afya kaya masikini.
Mwenyekiti wa Halmashauri kuu Taifa ya bakwata na mwenyekiti mwenza wa ISCEJIC Shekher Hamisi Mataka(katikati) kushoto ni Askofu Mkuu kanisa la Mennonite, kulia ni Shekher kabeke.
Takribani Watanzania milioni 3 ni masikini wa chakula hali iliyopelekea Taasisi hizo kuiomba Serikali kuwalopia Bima ya AFya ili kuhakikisha huduma ya Afya ya Bima inafanyika kwa watu wote nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Halmashauri kuu Taifa ya Bakwata na mwenyekiti mwenza wa ISCEJIC,Shekher Hamisi Mataka amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine ihakikishe Watanzania wanaelewa na wanahimizwa kujiunga na Bima ya Afya iliyoboreshwa.
Aidha Serikali ijitahidi kuongeza wigo wa wa kulipa kodi na pia kutenga kodi maaalimu kwa ajili ya kugharamia buruma za Afya kwa kaya masikini.
"Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na majadiliano mbalimbali hasa kuhakikisha kuwa sheria ya Bima kwa wote " amesema Shekher Hamisi.
Kwa upande wake mwenyekiti mwenza wa dini mbalimbali Askofu Mkuu kanisa la Mennonite Nelson Kisare ameeleza kuwa ni vyema msaada huo kupelekwa bungeni ili kuwe na sheria ya Bima kwa watu wote.
Anasema wanaomba sheria hiyo ipitishwe au kusomwa kwa mara ya kwanza Bungeti ili iletwe kwa wadau kujadili kwa kina.
"Viongozi wa dini tumefarijika zaidi kuona maendeleo wa dhamira nzuri ha Serikali juu ya masuala ya Bima za watu wetu,please ambapo Waziri wa fedha katika hotuba yake ya bajeti ya Taifa ya mwaka 2021/2022 ukurasa wa 69,amesema kuwa Serikali imetenga bajeti ya takribani Bilioni 150 kila mwaka kwa ajili ya kulipia kaya masikini Tanzania" amesema Kisare.
Hata hivyo mratibu wa Taasisi hiyo Edmund Matotay amesema kuwa Taasisi hiyo imeanza mwaka 2017 huku utafiti wa kupigia kampeni ya ya Uboreshaji huduma za Afya nchini umeanza mwaka 2018 ambapo viongozi wa dini wamekuwa waliendelea kama jukumu lao la asili katika maeneo yote wanayofanyia kazi tangu kuja kwa imani za dini.
Mwisho
No comments