OFISI YA MBUNGE NYAMAGANA YAPONGEZWA KUWAKUMBUKA WATOTO WENYE ULEMAVU.
Na Tonny Alphonce,Mwanza.
Shule ya msingi Buhongwa iliyoko wilayani Nyamagana
Mkoani Mwanza imeishukuru ofisi ya mbunge jimbo la Nyamagana kwa kutoa fedha za
ujenzi wa matundu kumi ya Choo utakayozingatia uwepo wa
wanafunzi wenye ulemavu shuleni hapo.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Buhongwa Oliver Benedicto akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa matundu 10 ya Choo katika shule ya Buhongwa Mwanza.
Akizungumza mbele ya kamati ya mfuko wa jimbo la Nyamagana jiji la Mwanza Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Buhongwa Oliver Benedicto amesema msaada huo wa ujenzi wa mashimo 10 ya choo utamaliza tatizo la msongamano wa wanafunzi Chooni.Mwalimu Oliver amesema shule ya msingi Buhongwa inakitengo
cha wanafunzi wenye ulemavu na wale wenye mahitaji maalumu hivyo kukamilika kwa
Choo hicho kutasaidia wanafunzi kujisaidia bila tatizo lolote kutokana na
miundombinu kuwa rafiki kwa wanafunzi wenye ulemavu.
“Kiukweli tunamshukuru sana Mh Mbunge Stanslaus
Mabula kwa kutupatia sh.milioni 5 kwaajili ya ujenzi wa Choo hiki ambapo hadi
sasa ujenzi umefikia asilimia 70 na bahati mbaya fedha zimeisha na tunamuomba
Mbunge au wadau wengine watupatie kama milioni 4 ili tukamishe ujenzi wa Choo
hiki”.alisema Mwl Oliver.
Akizungumzia faida watakazozipata wanafunzi mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Choo hicho,Mwl Oliver amesema kutapunguza uhaba matundu ya Vyoo kwa wanafunzi wa kawaida na wale wenye ulemavu,kutafanya watoto wawe kwenye mazingira salama ya kujistiri na kutaimalisha afya za wanafunzi kwa kujisaidia katika mazingira safi hasa kwa upande wa wanafunzi wenye ulemavu wa madarasa ya awali.
Akizungumzia miundo mbinu ya shule ya msingi Buhongwa
kwa wanafunzi wenye ulemavu Mwl Mkuu Oliver Benedicto amesema mazingira awali
hayakuwa rafiki na shule imeanza kubadili miundombinu taratibu kila inapoongeza
majengo mapya ili yaweze kutumiwa pia na wanafunzi wenye ulemavu.
“Serikali imeliona matatizo wanayopata wanafunzi
wenye ulemavu na ndio maana majengo ya zamani tumeyaongezea ngazi
zitakazowawezesha hata wanafunzi wenye ulemavu waweze kuyatumia na kwa majengo
mapya kipaumbele chetu ni kuweka mazingira mazuri pia kwa Watoto wenye ulemavu”,alisema
Mwl Oliver
Kwa upande wa taaluma kwa wanafunzi wenye ulemavu na wale wa mahitaji maalumu Mwl Oliver amesema shule yake bado inauhitaji wa walimu kwa upande wa wanafunzi wenye mahitaji maalumu kwa kuwa waliopo hawatoshi.
Mjumbe wa mfuko wa jimbo la Nyamagana jiji la Mwanza Ramadhani
Salum amempongeza Mwl mkuu wa shule msingi Buhongwa kwa kutumia vizuri fedha za
mfuko wa bunge zilizotolewa na mh mbunge na kuahidi kulifikisha kwa mbunge ombi
la shule hiyo la milioni 4 ili kukalmilisha ujenzi wa Choo hicho.
Mjumbe wa mfuko wa jimbo la Nyamagana jiji la Mwanza Ramadhani Salum akielezea kuridhishwa kwake na hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa matundu 10 ya Choo katika shule ya msingi Buhongwa Mwanza.
Jovither Mwombeki mratibu wa lishe mkoa idara ya Elimu amesema wao kama mkoa kazi yao kubwa ni kuhakikisha wanafunzi wenye ulemavu kuanzia wa darasa la awali wanakuwa na mazingira rafiki ya kusomea sambamba na kusimamia ujenzi wowote mpya uzingatie usawa kwa wanafunzi wote.Akizungumzia kauli mbiu ya Siku ya Walemavu ya mwaka huu inayosema Si kila
ulemavu unaonekana Jovither amesema ni jukumu la walimu kuwa makini
wanapowafundisha Watoto na kujitahidi kuwanao karibu ili kujua mapungufu yao
kwa kuwa kuna wanafunzi wanaweza kuwa na ulemavu uliojificha.
No comments