Aweso awafunda Maafisa Manunuzi
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Maafisa manunuzi wa Mamlaka za Maji Nchini wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano hali itakayosaidia kurahisisha utekelezaji wa miradi ya maji kukamilika kwa wakati.
Rai hiyo imetolewa leo Desemba 13,2021 na Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso wakati akifungua kikao cha Maafisa Manunuzi wa Mamlaka ya Maji kilicho lenga kujadili utendaji kazi ambacho kimefanyika Jijini Mwanza.
Amesema kuwa ili maafisa Manunuzi waweze kufikia kwenye malengo mbalimbali waliyojiwekea wanapaswa wafanye kazi kwa bidii, wawe na nidhamu kazini pamoja na ushirikiano.
"nitoe wito kwa baadhi ya Maafisa Manunuzi mjitahidi sana kukamilisha utaratibu wa Manunuzi ili shughuli ziwe zinatekelezwa kwa wakati, mnapo chelewa kwa kigezo cha kufanya mchakato wa Manunuzi usio kamilika mnasababisha miradi kushindwa kukamilika kwa wakati",amesema Aweso
Kwa upande wake Afisa Manunuzi kutoka Luwasa Korogwe, Halima Mhando amesema kuwa ameyapokea maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri wa Maji ikiwemo kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuweza kuhakikisha kazi za kutekeleza miradi zinasonga mbele.
Mwishoooo
No comments