Wazazi washauriwa kuwawekea akiba watoto wao
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala akizungumza na wanafunzi wa Shule mbalimbali na vyuo katika viwanja vya furahisha kwenye kilele cha wiki ya akiba duniani
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Wazazi wameshauriwa kujenga utamaduni wa kuwaweka akiba watoto wao ambayo itawasaidia hapo baadae ni vema kuwashirikisha watoto na walimu ili kuweza kufahamu umuhimu wa utunzaji akiba.
Hayo yamesemwa katika kilele cha wiki ya kuweka akiba dunia Mkoani Mwanza katika viwanja vya furahisha iliyoudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wanafunzi kutoka shule mbalimbali.
Baadhi ya viongozi walio hudhuria katika kilele hicho wamewaasa wananchi kujifunza kuweka akiba kwani imekuwawepo tabia kwa baadhi ya wananchi I kutokujali kesho yao na kuanza kuomba misaada inayotolewa kwa masimango hivyo ni vema tunaendelea kuelimisha njia sahihi ya uwekaji akiba.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika lisilo la kiserikali kutoka Nchini German DSIK Tanzania Stephen Safe alipokuwa akizungumza katika mkutano huo alisema kuwa ilikuondokana na mitazamo hasi ni kuondokana na misemo isiyokuwa na tija iondolewe ilikusaidia kizazi cha baadae kuwa na muamko wa kuweka akiba.
"Tupo kwenye hatua ya mwisho tuweza kuonana na wizara husika ya Tamisemi tuingie rasmi mashuleni kwani tayali vitabu vyetu vya elimu ya fedha vimepata baraka zote kutoka Tanzania institute education alisema mkurugenzi Safe.
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoawa Mwanza Muhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala alisema kuwa,ilikufikia malengo ni lazima kuweka akiba ilikufikia ndoto yako.
"Wakati huu tunaposherehekea siku ya uhamasichaji ya uwekaji akiba duniani tukumbuke kwamba huwezi kupata kitu au ndoto yako bila kuweka akiba hivyo uwe mtoto au mkubwa tujifunze kuendelea kuweka akiba ili kutimiza ndoto yako ya baadae tuache tamaa tuwe waelevu alisema masala",
No comments