Breaking News

Wahitimu CBE washauriwa kuwa wabunifu



Na Hellen Mtereko, Mwanza

Wahitimu wameshauriwa kuwa na maadili mema  ilikuweza kufikia malengo yao na kuendelea kuwa wabunifu kutokana na uhaba wa ajira hapa Nchini.

Hayo yamebainishwa na Katibu mkuu wa wizara ya viwanda na biashara Dkt.Dotto James alipokuwa akizungumza katika mahafali ya 14 ya  chuo cha  elimu ya biashara  kampusi ya Mwanza na mahafali ya 56 ya chuo hicho hapa Nchini.



Dkt.James amesema kuwa,kazi zipo isipokuwa wewe umejipangaje kuzifanya hizo kazi huwenda ni za kuajiriwa au kujiajiri na kuajiri wenzako  Taasisi za fedha zipo na wanahela za kukopesha isipokuwa mjipange muandike  andiko lenu vizuri hizi Benki zikishakuelewa haziwezi kukunyima fedha tuwe wazelendo ,heshima na maadili mema tujitume ili tufikie malengo ya kujenga Nchi yenye watu wasiokuwa tegemezi.

"Kuna kufanikiwa na kutofanikiwa kikubwa usikate tamaa tuvae uzalendo wenye heshima tupendane ndio tutakuwa na Taifa lenye maendeleo amesema Dkt.James.

Dkt. James ameupongeza uongozi wa  chuo hicho kwa kufanya  vizuri  na kuendelea kutoe elimu zaidi na mpaka sasa kinauwezo wa kudahili wanafunzi  2000 kutoka wanafunzi 400 hivyo  Serikali itaendelea kukitizama zaidi ilikuweza kumaliza changamoto ambazo wamezibainisha kikubwa tunataka kiendelee  kutoa wanafunzi wengi ili vijana wetu wapata elimu kama sera ya Serikali inavyotaka.

Mkuu wa chuo cha elimu ya Biashara (CBE)  Prof. Emmanuel Mjema amesema kuwa hatua wanazozichukua ilikuwaongezea uwezo wahitimu ni kuongeza mipango ambayo itawasaidia wanafunzi  kuanzisha biashara zao  zitakazosaidia kujiajiri  na tumeanzisha mpango mwingine wa mwanafunzi anasoma huku anafanya kazi tumeona wanafunzi wengi hawana ujuzi wa kufanya biashara kwahiyo kupitia mikakati hii tutawasaidia wanafunzi wetu kujiajiri zaidi na kuajiri wengine kikubwa waweze kunufaika na elimu wanayoipata hapa chuoni.

Wahitimu wa ngazi mbalimbali kutoka Chuo cha elimu ya biashara (CBE)kampasi ya Mwanza.

Prof.Mjema ameongeza kuwa, chuo cha  CBE kinajitahidi kutoa wanafunzi wenye weledi mzuri kwahiyo tunazidi kuishukuru Serikali kwa kutununulia eneo hili na majengo na sisi tutaendelea kufanya vizuri zaidi chuo hiki kimetoa watu wakubwa sana wakiwemo mawaziri, wafanya biashara wakubwa kwahiyo hakuna kitakachoturudisha nyuma na kushindwa kuwasaidia na kuwapa ujuzi vijana wetu wenye ndoto kubwa ilikuinua Nchi yetu.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa bodi ya uongozi wa chuo cha elimu ya Biashara Prof Wineasta Anderson amesema lengo kubwa la chuo ni kutoa wahitimu wanaojitambua katika tasinia mbalimbali ikiwemo ujasiliamali ilikutengeneza Taifa la watu wanaojitengemea ili mwanafunzi akimaliza masomo yake akaajiri watu wengine.

Amesema wahitimu wamepikwa vizuri   wataenda kuwa mabalozi wazuri ili wasiende kuwa tegemezi lakini chuo kina changamoto ambazo tunaomba Serikali iweze kututatulia zikiwemo za miundombinu ya barabara,umeme,na bweni ya wanafunzi linahitaji kufanyiwa ukarabati.

Jumla ya wahitimu 484 wametunukiwa Astashahada, Stashahada na Shahada wanaume 257 sawa  na 53% na wanawake 227 sawa na 47% .

Mwishoo

No comments