Breaking News

Waandishi wa habari kuimarishiwa ulinzi


Mkurugenzi Mtendaji wa umoja wa vyama vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Abubakar Karsan akifungua mdahalo wa ulinzi na usalama wa mwandishi wa habari uliofanyika Jijini Mwanza

Na Hellen Mtereko,

Mwanza

Umoja wa vyama vya waandishi wa habari  Tanzania (UTPC) Kwa kushirikiana na chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza (MPC) wameendesha mdahalo ulioshirikisha Jeshi la polisi kwa lengo la kuimarisha usalama kwa waandishi wa habari wanapokuwa kazini.

Akifungua mdahalo huo uliofanyika katika ukumbi wa Nyakahoja uliopo Jijini Mwanza, Mkurugenzi Mtendaji wa umoja wa vyama vya waandishi wa habari ( UTPC ) Abubakar Karsan amewataka Waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza kushirikiana  na Jeshi la polisi kutangaza habari kwa ufasaha ili kuweza kuleta ufanisi mzuri wa kazi hali itakayosaidia  kupunguza upotoshaji na taharuki kwa jamii.

Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza (MPC) Edwin Soko akitoa wasilisho la ulinzi na usalama wa mwandishi.

Amesema kuwa lengo la mdahalo huo nikuwafikia waandishi wote kote Nchini kwa lengo la kutoa elimu ya mahusiano mazuri Kati ya waandishi wa habari na jeshi la polisi baada ya kuibuka migogoro ambayo itaweza kusababisha  kukwamisha upatikanaji wa habari.

Akiwasilisha mada ya ulinzi na usalama katika mdahalo huo Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza  Edwin Soko amesema kuwa  mwandishi wa habari anahitaji ulinzi pindi anapokuwa anatekeleza majukumu yake ya kihabari hivyo ni muda sasa wa kushirikiana kikamilifu na Jeshi la polisi ili utendaji kazi uwe wenye tija zaidi.





Akiwasilisha mada kwa niaba ya kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza Ramadhan Ng'anzi,Mkaguzi Msaidizi  wa Jeshi la polisi dawati la habari Mkoa wa Mwanza  Oscar Msuya amekipongeza Chama Cha waandishi wa habari  Mwanza  kwa ushirikiano mzuri wanao uonesha kwa Jeshi la polisi katika kutekeleza majukumu yao ya kikazi.

Aidha amewaomba waandishi wa habari kutoa taarifa za uhakika ambazo haziwezi kusababisha uvunjifu wa amani na upotoshaji unaohatarisha usalama wa taifa.

Mwishooo

No comments