URATIBU MBOVU WA KESI ZA WATOTO CHANZO CHA KUKOSEKANA KWA HAKI ZAO.
Na Tonny Alphonce,Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Roberth Gabriel amesema pamoja na Mkoa wa
Mwanza kusimamia vizuri haki jinai lakini bado kunachangamoto upande wa
mahabusu, undeshaji wa kesi, uratibu wa kushugulikia kesi za watoto na mahakama
na hivyo kuwataka wajumbe wa Jukwaa la Haki Jinai kuhakikisha wanalitumia
jukwaa hilo kutatua changamoto wanazokumbananazo wadau na jamii kwa ujumla.
Mhandisi Roberth amesema kuna ukosefu wa uratibu mzuri wa kushunghulikia kesi za watoto na hivyo kesi nyingi za watoto huishia hewani na watoto wengi kukosa haki zao za msingi.
“Pamoja na kukosa uratibu wa kesi za watoto lakini tatizo lingine kubwa
linalowaathiri watoto ni ucheleweshwaji wa upelelezi katika kesi nyingi za
jinai hii hupelekea kesi nyingi kutofika mwisho”.alisema Mhandisi Gabriel.
Mhandisi Roberth Gabriel akizindua rasimi Jukwaa la Haki Jinai kwa Mkoa wa Mwanza.
Amesema kuzinduliwa kwa Jukwaa la Haki Jinai mkoani Mwanza kutatimiza
matakwa ya sheria hivyo kuhakikisha mkoa unaendelea kusimamia vizuri huduma za
haki jinai kwa makundi yoteJ
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi Mkoa wa Mwanza Rehema Mkinze amesema
kuzinduliwa kwa jukwaa hilo la haki jinai kutatua mashauri mbalimbali ya
wananchi na kuwataka wananchi nao kuhakikisha wanarahisisha kazi ya jukwaa.
Amesema kwenye kesi za watoto ni jukumu la Ustawi wa jamii,Magereza,Mahakama,Polisi Pamoja na Jamii kushiriki kuona haki za watoto waliona kesi zinapatikana.
“Jamii ina jukumu la kutoa ushaidi kwaajili ya kesi kwenda vizuri na
kuhakikisha haki inapatikana aidha kwa mtoto au kwa mtu mzima hivyo
tunamatumaini kupitia hili jukwaa ambalo linamchanganyiko la wataalamu kutoka
maeneo mbalimbali tunaona haki jinai itakwenda kupatikana.”alisema Rehema.
Amesema jukwaa hilo litakuwa na wajibu wa kutoa elimu pia kwa jamii
hususani upande wa kesi za watoto kwa kuwa jamii pia inaonekana haijui
kuhusiana na sheria ya Mtoto ambayo huelekeza usimamiaji wa kesi za watoto na
namna zinavyotakiwa kuendeshwa na hukumu zao zinavyotakiwa kuwa.
Kuzinduliwa rasimi kwa Jukwaa la Haki Jinai mkoani Mwanza kutaharakisha
utoaji wa haki mahakamani na kwa mahabusu.
No comments