UBALOZI WA MAREKANI:NEEMA YAJA KWA WAANAHABARI NCHINI
Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Bwana Donald Wright ameahidi kusaidia programu mbalimbali za habari ili kulinda uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari Tanzania.
Balozi Wright amesema hayo wakati alipotembelea klabu ya waandishi wa habari ya Mkoa wa Mwanza leo Novemba 10 na kufanya mazungumzo mafupi na viongozi wa MPC.
Baada ya Mwenyekiti wa MPC kuzungumzia changamoto za waandishi wa habari Tanzania ikiwemo uhitaji wa mafunzo, usalama na mazingira rafiki ya kufanyia kaza
Ndipo hapo Balozi Wright alipoeleza kwa kirefu kuwa atahakikisha anasaidia kundi la waandishi wa habari ili kuendeleza mazingira rafiki kwa vyombo vya habari.
Wright alisisitiza kuwa atakaa na wataalamu wake atakapo rudi Dar es salam na kuona uwezekano wa kusaidia baadhi ya programu za kuwajengea uwezo waandishi wa habari.
"Yote yaliyosemwa na MPC juu ya changamoto zinazowakabili waandishi wa habari na nitahakikisha nazifanyika kazi hivyo nawaahidi kuwasaidia'" Alisema Balozi Wright.
Mwenyekiti wa MPC Bwana Edwin Soko amesema kuna uhitaji mkubwa wa waandishi wa habari kijengewa uwezo kwenye maeneo muhimu kama usalama wa kimtandao kwa waandishi wa habari.
Pia Bwana Soko aliweka wazi juu ya changamoto ya takwa la kisheria ya ukomo wa elimu uandishi wa habari na kutoa pendekezo la kutazamwa upya kwa sheria hiyo huduma ya vyombo vya habari ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2017.
Mwandishi wa habari Florah Magabe aliongeza kuwa, waandishi wa habari wa kike wanahitaji kujegewa uwezo na pia kusaidiwa kwenye kuendesha blog zao kutokana na ada ya usajili kuwa kubwa.
Kabla ya ziara hiyo MPC imekuwa ikifanya kazi na taasisi zinazofadhiliwa na ubalozi wa Marekani ikiwemo shirika la Internews na Freedom House.
Balozi huyo alifanya mazungumzo mafupi na viongozi wa MPC na baada ya hapo alifanya mkutano na vyombo vya habari na wanachama wa MPC.
Mwisho...
No comments