TSC,TASAC wamefanya mkutano wa uhamasishaji kwa wadau wa usafirishaji.
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Baraza la wasafirishaji Tanzania (TSC)pamoja na Shirika la uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) wamefanya mkutano wa uhamasishaji kwa wasafirishaji kwa ajili ya kujadili namna ya uboreshaji wa sekta ya uchukuzi.
Mkutano huo imefanyika ukiwa na lengo la kuendeleza ushirikiano kati ya mdhibiti na wadau wa sekta inayodhibitiwa na Tasac Kama njia moja wapo ya kuinua uchumia kupitia sekta ya usafiri majini.
Akizungumza katika mkutano huo Meneja huduma za bandari Julius Mitinje, amesema kuwa kwa muda mrefu Tasac kwa niaba ya Serikali inatamani kuona wasafirishaji wa shehena Nchini Tanzania wakijengewa uelewa kadri mahitaji ya ujuzi na mbinu za biashara zinavyobadilika katika kusafirisha bidhaa nje ya Nchi ili kuweza kuendana na mabadiliko ya dunia hali itakayosaidia kuinufaisha Tanzania kwenye mizani ya malipo ya Nchi.
Amesema kuwa tija,ufanisi na mafanikio ya wasafirishaji shehena nje ya Nchi wanaathiliwa na utendaji wa watoa huduma mbalimbali katika sekta ya usafirishaji kwa njia ya maji, hivyo shughuli hii ni muhimu kwa sekta inayodhibitiwa na Tasac.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wa baraza la usafirishaji shehena Tanzania Ashraf Khan amesema kuwa, wasafirishaji wapatiwe elimu juu ya kuwa na nyaraka muhimu kabla ya usafirishaji mizigo,ununuzi ili kuondoa usumbufu bandarini na Mamlaka ya mapato Tanzania.
Amesema mategemeo yao bandari ni kuwa na tani million elf 20,000 kwa mwaka huu kutokana na Hali ya usafirishaji kuzidiwa kutokana na kupata meli za sarifa upande wa bandari zenye tani elfu 30,000.
Naye Program Menager kutoka -shipping ,ports& Freight services Aderick Kagenzi ameongeza kuwa, Katika tafiti zao wamebaini kuongeza uboreshaji,utendaji wa bandari na kuondoa vikwazo vya Kati ili bandari ya Dar es salaam iendelee kuwa lango kuu la bandari Africa Mashariki na Kati.
Akizungumzia upande wa tozo amesema kuwa Katika bandari siyo kubwa kwani wanaangalia namna ya kutoza tozo hizo kulingana na hali ya uchumi.
Amesema kuwa msafirishaji ili asafirishe mzigo wake ni lazima anaangalia unafuu wa safari ya kusafirisha mzigo, kwa kuangalia muda, usalama na ndio maana mizigo mingi inapita Bandari ya dar es salaam kutokana na uelekeo wa mzigo unapoenda.
Mwishooo
No comments