MDH KWAKUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA MAREKANI WAMEISAIDIA BUGANDO KUBORESHA MAABARA
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Shirika la Management and Development For Health (MDH) kwa kushirikiana na Serikali ya watu wa marekani wameisaidia hospitali ya Bugando kuboresha maabara ya kisasa itakayoweza kutoa huduma za upimaji wa covid19.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa maabara hiyo Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo Dr David Sando amesema kuwa uboreshwaji wa maabara hiyo ya kisasa umehusisha miundo mbinu, ununuzi wa vifaa, utoaji wa mafunzo rasmi kwaajili ya kujenga uwezo wa wapimaji sanjari na kuajili watu zaidi ya 15 watakao saidia kutoa huduma inayotakiwa.
Amesema kuwa MDH kupitia ufadhili wa watu wa Marekani wamekuwa wakisapoti huduma za maabara katika hosptali ya Bugando kwaajili ya kuhakikisha kwamba huduma zote za upimaji wa wingi wa virusi,upimaji wa virusi kwa watoto wachanga unafanyika kwa ubora unaotakiwa.
Sando amesema kuwa mwanzoni kabla ya huduma hiyo ya maabara wagonjwa waliohitaji vipimo vya covid19 walitakiwa kutoa sampuli ili zisafirishwe kwenda Dar es salaam na walikuwa wanapata majibu kwa muda wa masaa 72, lakini kwa sasa hivi kwa huduma hii kuletwa hapa karibu itapunguza changamoto ya kusubili majibu kwa muda mrefu.
"Tunajivunia sana Sapoti tunayoipata kutoka kwa Serikali ya watu wa Marekani na ushirikiano mkubwa ambao tunaupata kutoka kwenye hosptali ya Bugando kwani ushirikiano huo ndio unatuwezesha kuendelea kuboresha huduma za upimaji katika hosptali hii", amesema Sando
Balozi wa Marekani Donald Wright akitoa hotuba Mara baada ya kufungua maabara ya kisasa katika hosptali ya Kanda ya Bugando Jijini Mwanza
Kwa upande wake Mkurugenzi wa hosptali ya Kanda ya Bugando Dr Fabian Masaga amesema kuwa Wananchi wa Kanda ya ziwa na Tanzania kwa ujumla waeendelee kuiamini hosptali hiyo kutokana na inavyozidi kuboresha huduma katika nyanja zote za tiba,upasuaji na vipimo.
Amesema kuwa Serikali ya Marekani imetoa msaada mkubwa katika eneo la maabara na hivyo kutuwezesha kuweza kufanya vipimo vya Viral load Hiv, Hepatitis B, vina saba, Saratani pamoja na covid19.
Awali akizungumza Mara baada ya ufunguzi wa maabara balozi wa marekani Donald Wright amesema kuwa amefurahi sana kufika kwenye hospital ya Bugando na kuona utekelezaji wa maboresho ya maabala ya kisasa ambayo itakuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa Kanda ya ziwa kwa kupata vipimo mbalimbali.
Mwishoooo
No comments