Breaking News

lemela yafanikiwa kuwapanga machinga 3187 kwenye maeneo rasmi

Na Hellen Mtereko, Mwanza

Wafanyabiashara wadogo maarufu Kama machinga wapatao  3187 wamepangwa kwenye maeneo rasmi katika Halimashauri ya manispaa ya Ilemela.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa manispaa hiyo Modest Apolinary wakati akizungumza kwenye kikao cha  baraza la madiwani  cha robo ya  kwanza cha julai-Septemba cha  mwaka wa fedha 2021/2022.

Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza Cha robo ya kwanza juli - Septemba cha mwaka wa fedha 2021-2022


Amesema  jumla ya  wafanyabiashara wadogo  3187 wakiwamo wanaume 2345 na wanawake 842 wamefanikiwa kupelekwa kwenye masoko rasmi yaliyopo kwenye wilaya hiyo.

" Tumewapeleka kwenye masoko  mbalimbali yakiwamo Nyasaka,Kirumba,Buzuruga,Nyamanoro,Pasiansia,Buswelu kitangiri kwani zoezi hili linafanyika  sambamba na kuboresha miundo mbinu ya kuweka taa,maji  ",amesema Apolinary.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya  hiyo Hassan Masala amesema yoyote atakaye kutwa kwenye maeneo yasiyo rasmi anafanya biashara watamchukuliwa hatua za kisheria.

Naibu Waziri wa aridhi nyumba na maendeleo ya makazi, Angeline Mabula akizungumza kwenye baraza  la Madiwan
  

Naye Mbunge wa jimbo la Ilemela Dk Angeline Mabula ameishauri halmashauri hiyo kujenga eneo la machinga complex ili kuondoa changamoto ya wafanyabiashara kukosa maeneo.

Naye Diwani wa kata ya Ilemela Willbard Kilenzi  amewapongeza Mkurugenzi,Mkuu wa Wilaya kwa kufanya zoezi hilo kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali na kupelekea kufanikiwa bila changamoto yoyote.

Mwishooo.

No comments