BAKITA WAKITAMBUA RASIMI KITUO CHA KIMATAIFA CHA LUGHA (ICILD)
Na Tonny Alphonce, Mwanza
Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kwa kutambua mchango unaotolewa na Kituo Cha Kimataifa Cha Lugha,Utamaduni na Maendeleo limekitambua rasimi na kukikabidhi zana za kufundishia lugha ya kiswahili ili kuwarahisishia walimu.
Mchunguzi wa Lugha kutoka BAKITA Bwana Anord Msofe akizungumza na wageni waalikwa na wanafunzi wa ICILD wakati wa utambulisho rasimi wa kituo hicho.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kituo hicho mchunguzi lugha kutoka BAKITA Bwana Anord Msofe amesema Baraza linatambua mchango unayotolewa na vyuo vinavyofundisha Lugha ya kiswahili na Lugha za kimataifa kwa kuwa wanasaidia ukuaji wa lugha ya kiswahili.
Mkurugenzi wa ICILD kushoto,Mgeni Rsimi Bwana Ndassa na Mchunguzi wa lugha Bwana Msofe kutoka BAKITA tayari kukata utepe wa kuashilia kutambulika rasimi kwa kituo cha ICILD.
Kwa upande wa mkurugenzi wa kituo hicho cha ICILD Bwana Charles Mwombeki ameitaka serikali kuweka utaratibu kuweka sera itakayowataka wageni wote wanaoingia nchini kujifunza kwanza lugha ya kiswahili kabla hawajaanza kufanyakazi iliyowaleta hapa nchini.
Mkurugenzi wa kituo hicho cha ICILD Bwana Charles Mwombeki akisoma risala ya kituo hicho mbele ya mgeni rasimi.Mkurugenzi wa kituo cha ICILD Bwana Charles Mwombeki akipokea cheti cha kutambuliwa rasimi na Baraza la Taifa la Kiswahili Tanzania.
Kituo cha kimataifa cha Lugha,Utamaduni na Maendeleo ICILD hadi sasa kimetoa mafunzo ya lugha ya kiswahili kwa wageni zaidi ya 3000 na Watanzania zaidi ya 2000 wamejifunza lugha mbalimbali za kimataifa.
No comments