WATOTO WAZIPAMBA MBIO ZA ROCK CITY MARATHON
Na Tonny Alphonce,Mwanza
Watoto
wadogo wamejitokeza kwa wingi kushiriki mbio za Rock City Marathon na kuwa
kivutio kikubwa kwa watu waliojitokeza kushiriki na kushuhudia mbio hizo.
Akizungumzia
ushiriki wa watoto katika mbio hizo Dc Masala amewataka wazazi na walimu
kuangalia vipaji vya Watoto wanapokuwa nyumbani na shuleni na kisha kuchukua
hatua za kuendeleza vipaji hivyo kama ambavyo walivyowashirikisha Watoto katika
mbio hizo la Rock City.
“Serikali
inaendelea kuweka mazingira Rafiki katika michezo yote ikiwemo mchezo huu wa
riadha na lengo hapatunataka kuwaandaa vijana waweze kushiriki mashindano ya
kitaifa na yale ya kimataifa.”alisema Dc Msala.
Kwa upande
wake mzazi wa mtoto Joyce aliyeshiriki mbio hizo Martin Mahinde amesema mtoto
wake anapenda mchezo wa riadha na amekuwa akimruhusu kushiriki katika mbio
mbalimbali na matokeo sio mabaya kwa kuwa amekuwa hatoki katika nafasi ya kumi
bora.
Mbio za
Rock City Marathon hufanyika kila mwaka mkoani Mwanza ambapo mwaka huu Mtanzania
Alphonse Simbu ameibuka msindi wa mbio ndefu kilometa 21.
Mbio hizo
za Rock City Marathon ambazo zilidhaminiwa pia na KCB BANK zimeshirikisha
wakimbiaji zaidi elfu moja wakiwemo watoto na na watu wenye Ualbino.
No comments