WAOMBA HUDUMA YA MAJI WAPATE MUDA WA KUHUDUMIA FAMILIA:
Na Tonny Alphonce,Shinyanga
Wanawake wa
Kijiji cha Mwakilosa Mkoani Shinyanga wameiomba serikali kuwapatia huduma ya
maji safi ili waweze kupata muda wa
kuhudumia familia.
Wanawake hao
wamesema Kijiji chao kina shida kubwa ya maji kiasi kwamba inawabidi watembea
Zaidi ya kilometa 9 kutafuta maji kwaajili ya matumizi ya nyumbani.
Salome
Mchila mama wa Watoto wanne amesema Watoto wake wamekuwa na wakati mgumu wa
kupata kifungua kinywa kwa kuwa kila siku lazima aamke saa 10 alfajiri kwaajili
ya kwenda kutafuta maji ya kutumia.
“Mtoto wangu
wanne ana mwaka mmoja nimekuwa sipati hata muda wa kumnywesha uji wakati kwa
kuwa kila siku asubuhi lazima nitoke kwenda kutafuta maji na saa 9 alasiri
natoka tena kwenda kutafuta maji ndio maana nakosa hata muda wakukaa na Watoto
na kuwaandalia chakula kizuri”alisema Salome.
Amesema
wakati wa mvua ndio wamekuwa wakipata nafuu kidogo kwa kuwa wamekuwa wakitumia maji
ya mtaro
pale mvua zinapokuwa zimenyesha japo maji hayo bado kiusalama hayapo
vizuri na watu wengi wamekuwa wakiugua homo ya matumbo na kuharisha.
Naye mganga
mfawidhi wa Zahanati ya Mwakilosa Dkt Antony Marwa amesema takwimu zinaonyesha
kuwa katika wagonjwa 10 wanaofika kupatiwa matibabu katika zahanati hiyo wanane
kati yao wanasumbuliwa na ugonjwa matumbo na kuhara wakiwemo Watoto wenye umri
wa mwaka 02 – 15.
“Tunajaribu
kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kuchemsha maji ya kunywa lakini hawafanyi hivyo
Pamoja na kuwa wanachota haya maji katika vyanzo vya maji ambavyo havipo salama
hivyo wagonjwa wanaougua magonjwa yanayotokana na ukosefu wa maji salama ni
wengi hapa”alisema Dkt Marwa.
Kwa upande
wake Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary amesema tayari serikali imeishatenga fedha kwaajili ya kutatua tatizo la maji katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Shinyanga.
Amesema mradi maji kutoka Ziwa Victoria tayari unawasaidia wananchi wengi hasa wale waliokaribu na bomba hilo la maji na adha ya maji waliyokuwanayo imebakia historia.
No comments