Breaking News

UCHANJAJI WA CHANJO YA UVIKO 19 UNAENDELEA VIZURI MKOANI MWANZA

 Na Annastazia Maginga,Mwanza.


Takribani watu  elfu 28 wamefanikiwa kuchanjwa chanjo ya UVIKO 19 Mkoani Mwanza.

Akizungumza kwenye mdahalo  waandishi wa habari Mganga Mkuu wa Mkoa Thomas Rutachunzibwa, amesema muitikio umekuwa Mkubwa tofauti na mwanzo kutokana na elimu inayoendelea kutolewa juu ya umuhimu wa chanjo ya UVIKO 19.
Mganga Mkuu wa wa Mkoa Thomas Rutachunzibwa akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari hawapo pichani.

Amesema Awali chanjo inaanza  walikuwa wakichanja watu 200  Hadi kufikia 1600 kwa sasa idadi hiyo inaendelea kuongezeka kutokana na wananchi kuendelea kupata uelewa juu ya umuhimu wa chanjo hiyo.

Aidha amesema maeneo ya vijini yamekuwa na muitikio Mkubwa kuliko mijini na kwamba vituo 346 ziko wazi kwa ajili ya huduma hiyo.

" Mwanzoni tulikuwa na vituo 27  lakini kwa Sasa tuna vituo 346  na niwaambie tu wananchi wajue hii chanjo  haina madhara kwa kiafya hivyo wale ambao hawajachanja naomba wajitokeze kuchanja" amesema Rutachunzibwa.

Baadhi ya Waandishi wa Habari wa mkoa wa Mwanza wakimsikiliza kwa makini Mganga Mkuu wa Mkoa Thomas Rutachunzibwa.

Amesema lengo la  Serikali ni kuhakikisha taifa linafikia asilimia 60 ya watu waliochanjwa kote nchini.

No comments