TCB imedhamiria kuwainua wanawake kiuchumi.
Benki ya Biashara ya Tanzania(TCB) imedhamiria kuwainua wanawake kiuchumi kwa kuwasaidia kuwa wajasiriamali shupavu kupitia shughuli mbalimbali wanazozifanya.
Hayo yalisemwa na kaimu afisa mtendaji Mkuu(TCB) Moses Manyatta wakati akizungumza na wafanyabiashara 400 kwenye ufunguzi wa kongamano la tatu la wanawake Jijini Mwanza lililoandaliwa na benki hiyo.
Alisema kuwa lengo la kufanya makongamano ya akina mama ni kusaidia kuongeza mchango wao katika uchumi wa Taifa kupitia fursa mbalimbali zinazopatikana katika benki ya Tcb ikiwemo mkopo wanaopata kwaajili ya kundeleza biashara zao.
Aliongeza kuwa dhamira kubwa ya Benki hiyo ni kuwaelimisha wajasiriamali jinsi ya kufanya biashara zenye tija hali itakayowasaidia kujikomboa kiuchumi.
Manyatta alisema kuwa hadi sasa akinamama ambao ni nusu ya wateja milioni moja wa Tcb wamekopeshwa zaidi ya bilioni 120 ambazo wanazitumia Kama mitaji katika kukuza biashara zao.
Naibu Waziri wa aridh Nyumba na maendeleo ya makazi Angeline Mabula akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mwanza.
Kwaupande wake Maimuna Kanyamala ambae ni mshiriki katika kongamano la kinamama alisema kuwa Benki hiyo imekuwa msaada mkubwa kwake kwani imempa mkopo ambao umemfanya kuwekeza katika kilimo.
"Benki ya Tcb ilinikopesha milioni tano ambazo zilinisaidia kuanzisha kilimo cha ndizi na pasheni,pamoja na kujenga banda la kukaa vibarua wanaonisaidia shambani ",alisema Kanyamala
Alitoa wito kwa wakinamama kuwa wasikae nyumbani kusubili kuletewa bali wachangamkie fursa zilipo kwenye benki ya biashara ya Tanzania(TCB) ili waweze kupata elimu pamoja na mikopo.
Naibu Waziri wa aridh Nyumba na maendeleo ya makazi Angeline Mabula kulia akikata utepe ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa kongamano la 3 la wanawake na biashara.
Awali akizungumza katika kongamano hilo Naibu Waziri wa aridh Nyumba na maendeleo ya makazi Angeline Mabula alisema kuwa Mkoa wa Mwanza asilimia kubwa wakinamama wanajishughulisha na biashara kwaajili ya kujipatia kipato.
" Pamoja na kinamama kujishughulisha na biashara zile fursa za kibenki walikuwa hawazipati sana kulingana na riba kuwa kubwa lakini kwa sasa kutokana na maelekezo ya benki kukuu benki zote zimeelekekwa kushusha riba zao na ndio maana benki ya biashara ya Tanzania imeanza na itashika kundi kubwa la watu kwani mkopo wenye riba nafuu ni fursa kubwa sana katika kukuza biashara.
No comments