TAMASHA LA MARAFIKI WA JEMBE:ATAKAKUNYUKWILE WAIBUKA KIDEDEA
Na Judith Ferdinand,Mwanza.
Timu ya kikundi cha Atakanyukwile imeibuka kidedea baada ya kuifunga timu ya kikundi cha Pasiansi goli 3-0, katika mchezo wa fainali wa tamasha la Marafiki Jembe,uliotimia vumbi katika uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza.
Mratibu wa tamasha la Marafiki Jembe Mrisho Mabanzo,akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mwanza,juu ya tamasha hilo.picha na Judith Ferdinand.
Tamasha hilo la marafiki Jembe liliandaliwa na Jembe FM,kwa lengo la kuwaleta pamoja vikundi vya kusaidiana kwenye shida na raha na vikoba katika siku ya kupambana na umaskini duniani,ambalo lilikuwa na michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu,riadha, ngoma,kukimbiza kuku na kuvuta kamba pamoja na burudani mbalimbali.Atakanyukwile ilifunga magoli hayo kupitia mshambuliaji wake Steve Marco aliyefunga magoli 2 huku Ally Ally akifunga goli moja.
Katika mchezo mwingine wa riadha upande wa wazee,Mgasi Mtengozi kutoka kikundi cha Pasiansi aliibuka mshindi akifuatiwa na Juvenary Kumbi huku Hakimu Katabazi akishika nafasi ya tatu
Riadha wanawake nafasi ya kwanza ilienda kwa Antonia Didas kutoka kikundi cha Tumaini group akifuatiwa na Belina Benedictor huku nafasi ya tatu ikishikwa na Angelina Haruna.
Hata hivyo riadha wanaume Joseph Robert kutoka kikundi cha Atakanyukwile aliibuka kidedea akifuatiwa na Fredrick Boniface akifuatiwa na Sebastian Ibrahim.
Aidha katika mashindano ya ngoma za asili kikundi cha Tumaini group kiliibuka kidedea baada ya kupata kura 38, kikifuatiwa na umoja wa Atakanyukwile kura 35, huku Uwebwe kikipata kura 32 na nafasi ya nne ilienda kwa Pasiansi Tupendane kura 21.
Kikundi cha Tumaini group kilichoibuka kidedea katika mashindano ya ngoma za asili katika tamasha la Marafiki Jembe,baada ya kupata kura 38, kikifuatiwa na umoja wa Atakanyukwile kura 35, picha na Judith Ferdinand
Akizungumzia tamasha hilo,Mratibu Marafiki Jembe Mrisho Mabanzo,amesema walifanya tathimini na kuona vikundi hivyo vinasaidia jamii moja kwa moja hivyo waliona siyo vibaya kuwaleta pamoja,wakafurahi pamoja wakabadilishana uzoefu.
"Katika kampeni yetu ya kupambana na umaskini,tumebaini kuwa vikundi hivyo ndiyo vyanzo vya kupambana na umaskini kwa maana wakisaidiana mtu mmoja mmoja hiyo ni njia ya kumshinda adui maskini ndio maana tukaja na kampeni ya marafiki Jembe,njoo tushare upendo, na hii ni mwaka wa kwanza na wataendelea kufanya hivyo mwaka ujao,"amesema Mabanzo
Mwendeshaji wa kipindi cha kikoba kutoka Jembe FM Anatoria Palali, amesema zaidi ya watu 700 wamewafikia katika vikundi vitano ambao wameshiriki katika semina na tamasha hilo.
Mwendeshaji wa kipindi cha kikoba kutoka Jembe FM Anatoria Palali, akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mwanza,wakati wa tamasha la Marafiki Jembe lililofa.picha na Judith Ferdinand.
Tamasha hilo la marafiki wa Jembe lililoandaliwa na Jmbe Fm mbali ya kuwakutanisha wananchi pamoja katika michezo mbalimbali,kula pamoja lakini pia liliwapatia elimu ya kujikomboa kiuchumi ili iweze kuwasaidia kimaisha.
No comments