Rc Gabriel:andaeni maeneo kwa wamachinga ambao hawajapata
Na Hellen Mtereko,Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza mhandisi Robert Gabriel ametoa wito kwa timu ya jiji wanaoratibu shughuli za upangaji wa wamachinga kuhakikisha wanamaliza kazi hiyo haraka ili wamachinga waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku.
Hayo aliyasema ofisini kwake wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkoani hapa.
Alisema amepokea maombi ya machinga wanaofanya biashara zao kwenye maeneo ya barabara ya soko la Buhongwa kuondoka maeneo yasiyo rasmi ifikapo Novemba 10 kwani watakuwa wameshakamilisha ujenzi wa vizimba katika maeneo waliyopangiwa.
Hata hivyo alisema serikali imetoa maeneo bure ili wafanyabiashara hao waweze kujitafutia kipato.
"Mkibaini kuna watu,kikundi kinawaomba fedha ili mpate maeneo toeni taarifakwa uongozi ili tuweze kuwachukulia hatua za kisheria",alisema Gabriel
Aidha, alilitaka shirika la umeme Nchini(TANESCO) kuhakikisha wanafanya taratibu za kuweka umeme na kuainisha maeneo ambayo wafanyabiashara hao watachukua umeme na kuingiza katika vizimba vyao.
Mwisho aliwaasa wamachinga kuendelea kujikinga na ugonjwa wa uviko 19 sanjari na kupokea chanjo mpya ambayo serikali ya Mkoa imepokea baada ya zile za awali kumalizia.
Mwishooooo
No comments