MTOTO KUJISAIDIA HAJA NDOGO NA KUBWA BILA KUJITAMBUA NI DALILI YA UGONJWA WA AFYA YA AKILI.
Na ANNASTAZIA Maginga,Mwanza.
Imeelezwa kuwa kitendo cha mtoto kujisaidia haja ndogo na kubwa bila yeye mwenyewe kujitambua ni moja ya dalili ugonjwa wa Afya ya akili.
Dkt Gema mesema baadhi ya watoto wenye matatizo ya afya ya akili wamekuwa Katika hali ya utundu,na kutotulia darasani hali inayopelekea baadhi ya wazazi kushindwa kugundua haraka kama mtoto anatatizo la ugonjwa wa Afya ya akili.
Aidha amewaomba wazazi na walezi kuwapeleka hospitali watoto wenye ugonjwa wa akili hospitali ili waweze kupatiwa matibabu ili kuwapunguzia tatizo hilo watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa huo na mwisho waweze kuishi vizuri kama watoto wengine.
Dkt Gema amesema kisayansi inaonekana matatizo ya Afya ya akili huanza wakati wa ujauzito ambapo umaskini na lishe duni ni Moja wapo ya sababu ya Ugonjwa wa Afya akili.
Dkt ameongeza kuwa asilimia 80 ya Ugonjwa huo ni wa kurithi na kwamba asilimia 50 ya watu wazima wenye ugonjwa huo hutokea Kabla ya kufikisha umri wa miaka 14.
Awali akizungumza kwenye uzinduzi huo wa kuelekea siku ya maadhimisho ya Afya ya akili duniani ,Mkuu wa Idara hiyo Kiyetia Hauli, amesema wagonjwa 30 hadi 70 wamekuwa wakipata huduma kwa siku Katika hospitali ya Rufaa ya Bugando.
Mkuu wa Idara ya Afya ya akili hospitali ya Bugando Dr. Kiyetia Hauli akitoa neno wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya Afya ya duniani huku kilele chake kikiwa tarehe 10/10/2021.
Uzinduzi huo kwa mwaka huu umeambatana na kauli mbiu isemayo Afya ya akili Katika Ulimwengu usio na usawa ikimaanisha kwamba huduma hizo hutolewa Katika sehemu za mijini na sio vijijini hali ambayo haileti usawa Katika utoaji wa huduma.
No comments