Mkoa wa Mwanza umetajwa kuwa sehemu salama ya kufanyia biashara.
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Wafanya biashara wa Mikoa jirani wameombwa kuendelea kuwekeza na kufanya biashara zao katika Mkoa wa Mwanza ili waweze kukuza mitaji yao kutokana na Mkoa huo kuwa sehemu salama ya kufanyia biashara.
Ombi hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel wakati alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara pamoja na wawekezaji katika hafla fupi ya Ufunguzi wa tawi jipya la kampuni ya Silent Ocean inayojihusisha na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali kutoka China na Dubai.
Gabriel alisema kuwa wawekezaji wanaokuja kuwekeza katika Mkoa wa Mwanza wasinyanyaswe Wala kuzungushwa wala kusiwepo dalili zozote za kuwaomba rushwa,pia alisema kuwa ofisi yake iko tayari kutoa ushirikiano kwa wafanyabiashara kwani nia yake ni kutaka kuona Mwanza inakuwa ni kitovu cha biashara.
Alisema kuwa wafanyabiashara wanatumia mitataji yao, wanakopa fedha ili kuweza kuwekeza katika biashara na wamekuwa wakileta mapinduzi yakiuchumi kuanzia kwenye familia zao na Taifa kwa ujuma.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa masoko na mauzo kutoka kampuni ya Silent Ocean Mohamed Kamilagwa,alisema kuwa wamekuja kufungua tawi jipya Mwanza kwa lengo la kusogeza huduma kwa wafanyabiashara ambao wako Kanda ya Ziwa ili kuwapunguzia wateja wao gharama za usafiri kwenda Dar es alam kufata bidhaa.
Alisema kuwa biashara ya usafirishaji kunaushindani mkubwa Sana na kampuni hiyo wamekuwa Kama viongozi katika huo ushindani kwa kufanya mambo bora zaidi kwenye tekinolojia na kwakuongeza matawi mengine lengo ikiwa ni kurahisha upatikanaji wa bidhaa kwa wateja.
Kamilagwa alisema kuwa kwa Kanda ya Ziwa wanawateja wasiopungua 900 ambao wanafanya nao kazi na wamekuwa wakijitahidi sana kutoa huduma bora ya kusafirisha bidhaa za wateja wao kwa usalama mkubwa na ndio kigezo pekee cha kuaminiwa na watu mbalimbali Nchini.
Alisema kuanzishwa kwa tawi hilo kutakuwa na faida ya kiuchumi kwani wafanyabiashara wataongezeka na mzunguko wa biashara utakuwa mkubwa hali itakayosaidia Serikali kukusanya mapato kwa wingi.
Alisema kuwa ujio wa tawi hilo ni fursa kubwa Sana kwa wafanyabiashara hivyo waitumie vyema ili waweze kujiinua kiuchumi,aliongeza kuwa kwa sasa wanawateja zaidi ya 900 lakini malengo yao wanatarajia ifikapo mwaka 2022 wawe wamepata wateja 2000.
Juliana masabu ni mmoja wa wafanyabiashara aliehudhuria hafla hiyo alisema kuwa amefurahi Sana kuanzishwa kwa ofisi ya Silent Ocean kwa hapa Mwanza kwani itawasaidia kupata bidhaa zao kwa haraka ukilinganisha na zamani walivyokwa wakisafiri kwenda dar es alaam.
Mwishoooo
No comments