Breaking News

Kuelekea kilele cha wiki ya akiba DSIK yafanya mdahalo kuhusu elimu ya fedha




Na Hellen Mtereko,

Mwanza

Kuelekea kilele cha wiki ya akiba duniani shirika lisilo la kiserikali linalofadhiliwa na Serikali kuu ya Ujerumani  German Sparkassenstiftung Eastern Africa (DSIK), linalojihusisha katika kusaidia sekta ndogo za fedha duniani kote kwalengo la kukuza maendeleo endelevu ya kiuchumi limekutana na wadau mbalimbali Jijini Mwanza kwa lengo la kufanya mdahalo.

Akitoa hotuba katika mdahalo wenye mada isemayo 'Nini mchango wa jamii katika kuimarisha elimu ya fedha na utamaduni wa kujiwekea akiba kwa Watoto na vijana' Mkurugenzi Mkazi wa DSIK Tanzania Stephen Safe alisema kuwa lengo la kufanya mdahalo huo Ni kukumbusha juu ya kuweka akiba na matumizi mazuri ya fedha.

Alisema kuwa wamekuwa wakitoa elimu ya fedha katika Jamii kwa kushirikiana na ushirika wa taasisi ndogondogo za kifedha Nchini(TAMFI),mfuko wa SELF MF, Tume ya maendeleo ya ushirika(TCDC) pamoja na Muungano wa vyama vya ushirika wa akiba na mikopo (SCCULT).

Safe alieleza kuwa DSIK kwa muda wa miaka mitatu imekuwa ikitoa elimu ya fedha kwa Mkoa wa Mwanza na wanategemea hivi karibuni kuanza kutoa elimu hiyo kwenye shule za Serikali ili kuweza kuwafundisha wanafunzi umuhimu wa kuweka akiba.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mdahalo wa elimu ya fedha pamoja na viongozi kutoka shirika la DSIK katika ukumbi wa Chuo cha Benki kuu Mwanza

Alisema kuwa pamoja na kuchangia katika kuongeza ushirikishwaji wa kifedha na kutokomeza umasikini katika Jamii DSIK Tanzania inakutana na changamoto mbalimbali katika utoaji elimu ya fedha kwa wanafunzi ikiwemo uelewa mdogo wa masuala ya fedha kwa jamii, wazazi na walezi.

"Familia nyingi hazina bajeti ya familia bali bajeti anayo Mkuu wa Nyumba na haizungumzwi mbele ya familia nzima, Shule na vyuo vingi kutofundisha elimu ya fedha na elimu ya fedha jumuishi Kama Somo au kilabu za wanafunzi sanjari na baadhi ya watu kuwazuia Watoto wao kujua elimu ya  fedha",alisema Safe

Aliongeza kuwa DSKI imeamua kutoa elimu ya fedha na elimu ya fedha jumuishi ili kuendana na malengo ya maendeleo endelevu ya umoja wa mataifa (Sustainable development goals), kwa kutoa elimu ya fedha pia tunachangia katika mpango wa maendeleo wa Tanzania 2025.

Akitoa mada katika mdahalo huo Dr Paulin Paul kutoka  Moshi Cooperative University-MoCU Mwanza Campus alisema kuwa Kuna umuhimu mkubwa wa kuitengeneza kesho yako kwa kujiwekea akiba.

Kwaupande wao viongozi wa dini walioshiriki katika mdahalo huo Askofu Mkuu Kanisa la wasabato Beatus Mlozi, Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Hassan Kabeke walisema kuwa wamekuwa mabarozi wazuri wakuwakumbusha waumini wao kuhusu kuweka akiba, na katika familia zao pia kuanzia kwa Watoto ili wakue wakijua misingi mizuri ya kujiwekea akiba katika maisha yao.

Awali akizungumza na kufungua mdahalo wa  uwekaji wa akiba Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel alisema kuwa elimu ya masuala ya fedha ni Kati ya nguzo muhimu katika Jamii na inawezesha  kupata uelewa wa jinsi gani mtu anaweza kupata fedha halali.

Alisema kuwa ukosefu wa elimu ya fedha umekuwa unaathiri rika zote katika Jamii lakini kwa Sasa Jamii inashuhudia Vijana wengi wanaoanza maisha kuwa na uelewa mdogo na nidhamu ndogo ya fedha hasa katika kufanya bajeti ya vipato vyao, jinsi gani waweze kudhibiti matumizi yao ili wasiingie kwenye madeni.

"Vijana wengi hawajui jinsi ya kujiwekea akiba ili iwasaidie wakati wa dharula na hii inatokea kwa Vijana wetu wa vyuo vikuu hapa Nchini pindi wanapoajiriwa au wanapoanza anza kazi, hivyo niwapongeze sana (DSIK) kwa hatua hii ya kuendelea kutoa elimu ya uwekaji wa akiba kwani ni msaada mkubwa sana katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla",alisema Gabriel

Mwishooo

No comments