Breaking News

COSTECH yawakutanisha Waandishi wa habari na watafiti.



Waandishi wa habari na watafiti kutoka Mkoa wa Kagera,Mara na Mwanza wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Menejiment ya Maarifa kutoka COSTECH

Na Hellen Mtereko, Mwanza

Watafiti mbalimbali Nchini wamekuwa wakifanya tafti katika masuala ya kisayansi lakini kazi zao haziwafikii Wananchi kutokana na kuwa na lugha ngumu ambayo ni ya kitafti hali inayopelekea kushindwa kufikisha taarifa hizo kwa Wananchi.

Hayo yamesemwa na mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia( COSTECH) katika mafunzo ya waandishi wa habari na watafiti,ambae pia ni Mkurugenzi wa Menejiment ya Maarifa katika Tume hiyo Dkt Philbert Luhunga.

Alisema kuwa ni muda sasa wa Waandishi wa habari kuandika taarifa za Sayansi, teknolojia na ubunifu na kuzitangaza kwa lugha rahisi inayotambulika na Wananchi jambo ambalo litaleta chachu ya maendeleo katika Jamii.

Luhunga alisema kuwa watafiti wamekuwa wakifanya tafti mbalimbali lakini Wananchi wanashindwa kupata taarifa sahihi za tatfi hizo, hivyo ni bora waandishi wa habari muandike matokeo ya tafti ili kuweza kusaidia kazi za watafiti wa Sayansi, teknolojia na ubunifu kutambulika na kutumiwa na jamii husika.

Kwaupande wake mtafiti mwandamizi kutoka katika taasisi ya utafiti wa uvuvi Tanzania(TAFIRI) Hillary Mrosso alisema kuwa Taasisi ya  COSTECH imekuwa msaada mkubwa sana kwao kwa kuwapa sapoti kwenye miradi mbalimbali.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi,teknolojia na ubunifu ambae pia ni Mkurugenzi wa Menejiment ya maarifa kutoka COSTECH  Philbert Luhunga akizungumza na wahandishi wa habari na watafiti katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Aliongeza kuwa COSTECH imewasaidia katika ujenzi wa miundombinu ya kiutafti,ikiwemo  majengo,mabawa, miradi ya kiutafti kwa maana ya kuwasaidia kupata taarifa sahihi katika sehemu husika,kuwapa mafunzo  pamoja na kuwasajili katika kuweka miongozo mbalimbali ya utafiti ambapo hadi sasa tumefanikiwa kukamilisha muongozo wa maadili ya utafiti.

Mrosso alisema kuwa kutokana na mafunzo ambayo wanaendelea kuyapata kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) wanaendelea kuielimisha jamii juu ya ufugaji bora wa vizimba ili waweze kuwa na ufugaji wenye tija.

Alisema kuwa ufugaji wa samaki unaeneo pana Sana katika kukuza uchumi wa buluu hususani kwa wale wanaofuga kwenye mabawa yenye maji mengi hivyo ufugaji huu unafaida kubwa sana kuanzia ngazi ya jamii na Taifa kwa ujumla.

Mwisho alitoa wito kwa wafugaji  kuwa pamoja na changamoto wanazokutananazo wasikate tamaa badala yake wawatumie wataalam ili waweze kuwapa ushauri juu ya maandalizi mazuri ya ufugaji.


Mwishooo

No comments