Breaking News

ALIYOSEMA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI, GERSON MSIGWA WAKATI AKITOA TAARIFA YA SERIKALI YA WIKI ILIYOFANYIKIA MKOANI MWANZA LEO OKTOBA, 2021

#Mwanza ni Mkoa wa pili nchini kuchangia fedha nyingi katika pato la Taifa, mwaka 2019 makusanyo ya mapato yalikuwa Trilioni 10.2 na hivyo kuchangia Pato la Taifa kwa 7.35% na mwaka 2020 yalikuwa Trilioni 10.9 hivyo kuchangia Pato la Taifa kwa 7.38.8%.

#Katika kipindi cha miezi 6, Serikali imeleta Mwanza shilingi Bilioni 344 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya wananchi ikiwemo Bilioni 219.1 ya kutekeleza miradi ya ujenzi ambapo Bilioni 44.7 zitatumika katika ujenzi wa Stendi ya Nyamhongolo na Nyegezi.

#Tunajenga Soko la Kisasa Mjini ambapo zimeshaletwa Bilioni 8, hadi kukamilika utagharimu Bilioni 20.3, zimeletwa Bilioni 4.5 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Abiria kwenye uwanja wa Mwanza ambapo ujenzi ukikamilika utagharimu shilingi Bilioni 13.3.

#Serikali imeleta shilingi Bilioni 18 kwa ajili ya ujenzi wa MV Mwanza yenye uwezo wa kubeba abiria 1,200 na tani 400 za mizigo, kazi imefikia asilimia 89. Ujenzi wa meli unatarajiwa kukamilika Mei, 2022 kwa gharama ya shilingi Bilioni 89.154.

#Serikali imeleta shilingi Bilioni 174 kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Kigongo – Busisi lenye urefu wa kilometa 3.2 pamoja na barabara za kuingia darajani zenye urefu wa kilometa 1.66, . Mradi huu hadi ukikamilika utagharimu shilingi Bilioni 699.278.

#Serikali imeleta Mwanza Bilioni 15.2, Bilioni 8.3 kwa ajili ya kujenga Hospitali 3 za Wilaya, kumalizia Hospitali 2 za Wilaya, kujenga Vituo vya Afya 5 na Zahanati 21,kukarabati na kujenga vituo vya huduma 48 pia zimeletwa Bilioni 6.4 za kununulia dawa.

#Serikali imeleta Mwanza Bilioni 38.7
 kwa ajili ya elimu ambapo Bilioni 11
 za miundombinu ya Shule za Msingi na Sekondari,Bilioni 8 
za elimu bila malipo. Tunatarajia kuleta Bilioni 19.7 kwa ajili ya kujenga madarasa 985.

#Serikali imeleta Bilioni 2.4 kwa ajili ya TARURA na TANROADS, imeleta Bilioni 42.6
 kwa ajili ya usambazaji wa Umeme kupitia REA,imeleta Bilioni 20.4
 kwa ajili ya miradi ya maji na Bilioni 5.6
 kwa ajili ya kusaidia Kaya masikini.

#Serikali inaendelea na dhamira yake ya kuliimarisha Jiji la Mwanza ambapo tayari imeshafanya mazungumzo na mwekezaji atajayejenga hotel ya kuelea majini katika Ziwa Victoria itakayosaidia kuvutia watalii na kupendezesha Jiji.

#Mradi wa ujenzi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere una Wafanyakazi Watanzania 7,713 sawa na 89% ya wafanyakazi wote 8,635. Mpaka sasa Wakandarasi wameshalipwa Trilioni 2.832 kati ya Trilioni 6. 558 zitakazotumika kugharamia ujenzi huu.

#Napenda kuwajulisha kuwa fedha zilizotolewa na IMF Shilingi Trilioni 1.3. Wizara ya Fedha na Mipango tayari imekamilisha maandalizi ya kugawa fedha hizo kwenda kwenye miradi husika ikiwemo ya kujenga madarasa 15,000, kununua madawati 462,795.

#Miradi mingine ni kujenga shule shikizi 3,000, kumalizia vyuo vya VETA 32, kununua magari ya wagonjwa 395, kununua vitanda vya hospitali 2,700, kununua xray mashine 85, CT Scan 29, mitungi ya gesi 4,640, kujenga ICU 72 na kununua mitambo 5 ya kuchimba visima vya maji

#Hadi Juni, 2021, TARURA imetumia Trilioni 1. 297 kutengeneza KM 24,979 za barabara, KM 955.35 kwa kiwango cha lami, KM 16,857 kwa kiwango cha changarawe pia wamejenga madaraja 231 na makalvati mapya 1,325. Mwaka huu wa fedha, Serikali imeitengea TARURA Bilioni 934.

#Serikali inajiandaa kutekeleza Mkakati wa Pili wa TARURA utakaoanza mwaka 2021/22 – 2025/26 utakaohusika na kuongeza barabara za lami kutoka KM 2,405 hadi KM 3,856, barabara za changarawe kutoka KM 29,116 hadi KM 102,358 na kuongeza madaraja kutoka 2,812 hadi 6,620.

#Uamuzi wa Serikali kuunganisha mifuko ya Hifadhi ya jamii na kuunda PSSSF umeleta mafanikio makubwa. Wastaafu ambao wanalipwa Pensheni kila mwezi,wanalipwa pensheni zao kabla ya tarehe 25. Septemba 2021 Wastaafu wamelipwa zaidi ya shilingi Bilioni 57.

#Wakati PSSSF inaanza kulikuwa na malimbikizo ya mafao ya wafanyakazi ya takribani miaka 3 na yalifikia Trilioni 1, lakini ndani ya miezi 6 yakawa yamelipwa. Kwa sasa PSSSF inakwenda na kauli mbiu ya “Lipa Jana” yaani mtu akistaafu leo apate mafao yake siku moja kabla.

#Wakati PSSSF inaanza kulikuwa na malimbikizo ya mafao ya wafanyakazi ya takribani miaka 3 na yalifikia Trilioni 1, lakini ndani ya miezi 6 yakawa yamelipwa. Kwa sasa PSSSF inakwenda na kauli mbiu ya “Lipa Jana” yaani mtu akistaafu leo apate mafao yake siku moja kabla.

#Takwimu za mpaka Oktoba 15, 2021 zinaonesha Watanzania 940,507 wamepokea chanjo ya UVIKO -19 sawa na 88.9% ya chanjo zote 1,058,400 aina ya JJ .
Shehena ya chanjo 1,065,000 aina ya Sinopharm zilizokuja kutoka China zimeanza kusambazwa katika Halmashauri na Mikoa yote.

#Tunatarajia kupokea chanjo aina ya Pfizer dozi 500,000 mwishoni mwa mwezi Oktoba kutoka COVAX FACILITY ambazo ni sehemu ya Dozi Milioni 3.7 za chanjo aina ya Pfizer ambazo nchi yetu itazipata kwa awamu kutoka COVAX FACILITY.

#Tayari majokofu ya baridi kali 14 yenye uwezo wa kuhifadhi chanjo zote Milioni 3.7 yameshafungwa pale Jijini Dar es Salaam.

#Ili kuhakikisha tatizo la kukatika kwa umeme mkoani Morogoro halijirudii, Serikali inajenga njia ya umeme Kilosa - Mikumi yenye urefu wa KM 25 itapeleka umeme wilayani Kilosa, inajenga pia njia nyingine ya KM 27 kutoka bwawani - Mikese pia inaendelea kuondoa nguzo chakavu.

#Mkoani Morogoro, Serikali inatekeleza mradi wa maji utakaogharimu takriban Bilioni 4, ujenzi wa tanki la maji la lita milioni 2 na mabomba yake, kujenga kituo kipya cha maji katika eneo la mizani na mashine mbili za kusukuma maji na kulaza mabomba ya mseleleko kutoka mto Morogoro.

#Serikali imetiliana saini na Shirika la Msaada la Maendeleo la Ufaransa kwa ajili ya kutekeleza mradi mkubwa wa maji utakaogharimu shilingi Bilioni 185 na utazalisha lita milioni 54,mradi huu utakamilika 2026

IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI - MAELEZO

No comments