Breaking News

MAONYESHO YA MADINI GEITA:WACHIMBAJI WADOGO WATANGAZIWA NEEMA NA NBC BANKI.


Na Tonny Alphonce ,GEITA

Meneja wa NBC mkoa wa Geita Hilda Bwimba amesema benki ya NBC itaendelea kutoa mikopo kwa wachimbaji wadogo  ili waweze kutoka kwenye uchimbaji wa kale na kuingi kwenye uchimbaji wa kisasa.

Ameyazungumza hayo wakati mkuu wa wilaya ya Geita alipotembelea banda la NBC ambapo Hilda alisema wachimbaji wadogo wamekuwa kuwa wateja wakubwa wa NBC na wamekuwa wakisaidiwa kwa kupewa mikopo.


NBC ambao ni wadhamini pia wa maonyesho hayo ya madini kwa mwaka huu wamehamishia pia huduma zao zote muhumu katika maonyesho hayo ambapo wananchi mbalimbali wamepata nafasi ya kufungua akaunti na kupata huduma zingingine za kibenki.


Wafanyakazi wa NBC wakimsikiliza kwa makini mteja aliyetaka kujua taratibu za kupata mkopo kutoka NBC zikoje na nani mwenye sifa ya kupata mikopo hiyo.

Mteja wa NBC akifurahia jambo na muhudumu wa NBC mara baada ya kufungua akaunti yake katika maonyesho ya madini yanayoendelea mkoani GEITA.

Maonyesho ya madini ambayo hufanyika kila mwaka mkoani Geita yameendelea tena mwaka huu yakiwa yamebeba kauli mbiu isemayo Sekta ya madini kwa ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu.





No comments