Wafanyabiashara wadogo watakiwa kurejea kwenye masoko
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala amewatoa hofu wafanyabiashara wa soko la Buzuruga kuwa miundombinu ya soko hilo itaendelea kuboreshwa ikiwamo kutenga sehemu ya mama lishe ya kumwagia maji taka.
Masala aliyasema hayo wakati alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi ya kutembelea masoko yenye lengo la kuwataka wafanyabiashara kurejea kwenye masoko waliyoyaacha wazi kwa muda mrefu.
Alisema kuwa lengo la Serikali ni kutaka kuona wafanyabiashara wanafanya biashara zao katika mazingira rafiki,ndio maana masoko yalijengwa ili kuweza kuepusha msongamano wa watu kulundikana barabarani.
Wafanyabiashara wakisikiliza maelekezo ya Mkuu wa Wilaya ya Ilemela@ Hassan Masala
" Mtakapo kuwa mmepangiwa sehemu za kwenda nendeni mkafanye biashara hatutaruhusu mtu yoyote kupanga barabarani wakati masoko yapo, Kuna athari nyingi Sana za kufanya biashara barabarani hivyo fateni maelekezo ya Serikali ili muweze kufanya shughuli zenu kwa amani",alisema masala
Aliongeza kuwa kila kitu kinakwenda kwa utaratibu sio kwamba mtakaporejea kwenye masoko hayo hamtapata wateja, watu watawafuata popote mtakapokuwa hivyo jipangeni taratibu Kama unakibanda hamisha ili usipate hasara kwa kile ulichowekeza.
Alisema , Machinga wanaofanya biashara zao ndani ya stendi wao wataendelea kufanya kwani hawazuii shughuli zingine kufanyika Wala hawazibi biashara za watu wengine hivyo wafanye kazi zao kwakufuata Sheria na taratibu zote za Nchi.
Hata hivyo kutokana na maagizo hayo ya kuwataka wafanyabiashara wote waliovamia katikati ya mji kurudi katika maeneo yao wanayostahili kufanyia biashara, Mkuu wa wilaya aliwataka Madiwani wa Halimashauri ya Ilemela kumpa ushirikiano kwani lengo ni kutaka kuona Wilaya hiyo inakuwa Safi.
No comments