Breaking News

VIJANA SINGIDA WATAKIWA KUZALISHA BIDHAA ZINAZOENDANA NA SOKO

 

Baadhi ya vijana mkoani hapa wakiendelea na ujenzi wa Kitaru Nyumba (Green House) baada ya kuwezeshwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia kampuni ya SUGECO,
Afisa Vijana Mkoa wa Singida  Frederick Ndahani akizungumza na vijana hao wakati walipokuwa wakiendelea na ujenzi huo.


Na Dotto Mwaibale, Singida


AFISA Vijana Mkoa wa Singida  Frederick Ndahani amewataka vijana kuzalisha bidhaa na malighafi zenye ubora unaokidhi soko . 

Ndahani aliyasema hayo jana alipokuwa akikagua mafunzo ya ufungaji wa vitaru Nyumba (Green House) yanatekelezwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia kampuni ya SUGECO,

Ndahani alisema kuwa vijana wengi wanajitahidi kujituma katika sekta mbalimbali ikiwemo uzalishaji wa mazao ya  kilimo ,mifugo na viwanda lakini tatizo limekuwa ni ubora wa malighafi na bidhaa hizo .

Ndahani amewataka vijana kuhakikisha wanatumia utaalamu na teckolojia za kisasa kuzalisha bidhaa Bora.

Ndahani alisema mkoa umeendelea kuweka jitihada kuhakikisha vijana wanapata mafunzo , kuwatafutia mitaji pamoja na masoko.

Alisema katika mkoa wa Singida  vijana wengi wanalima vitunguu  na tayari amekwishaongea na kampuni ya East Africa fruits iliyoko Dar es salaam kununua vitunguu vinavyozalishwa na vijana mkoani hapa ambavyo vinazalishwa kwa ubora unaendana na Soko la Afrika Mashariki.

Aidha Ndahani alisema mpango wa ukuzaji ujuzi kwa vijana kupitia kilimo cha Vitaru Nyumba utawanufaisha vijana 700 katika Mkoa wa Singida ambao watapata mafunzo ya kutengeneza Kitalu Nyumba na namna ya kulima kupitia mfumo huo wa kisasa.

Ndahani ameishukuru Serikali inayoongozwa na  Rais Samia Hassan Suluhu kwa kujali vijana wa Tanzania pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu kutekeleza mradi huo kwa ufanisi ili kuwasaidia vijana.

Ndahani ameahidi kushirikiana na vijana mkoani hapa ili waweze kujikwamua na umaskini kwa kuwa masoko ya mazao ya kilimo na ufugaji uliotokana na Singida kuwa karibu na makao makuu ya nchi yapo.

Kwa upande wao vijana wameishukuru Serikali ya awamu ya Sita kwa kuwapatia ujuzi  na mikopo ili kuondokana na umaskini.

No comments