Makamanda wa Polisi wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakutana na Wavuvi kujadili hali ya uhalifu Ziwani.
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Makamanda wa Polisi wa Mikoa ya Kanda ziwa, wakuu wa upelelezi, wakuu wa oparesheni pamoja na wadau wa sekta ya uvuvi wakutana Jijini Mwanza kwa lengo la kujiwekea mikakati ya kukabiliana na uhalifu ndani ya ziwa Victoria.
Akizungumza na waandishi wa habari Mara baada ya kufungua kikao kazi cha kujadili hali ya uhalifu ziwani,kamishina wa polisi Liberatusi Sabasi ambae pia ni kamishina wa oparesheni wa mafunzo Tanzania alisema kuwa dhamira Kuu ni kuhakikisha uhalifu ndani ya ziwa Victoria unakuwa historia.
Sabasi alisema kuwa kwa sasa uhalifu ndani ya ziwa Victoria umepungua kwa kiasi kikubwa sana, na hii ni kwasababu ya ushirikiano uliofanyika Kati ya jeshi la polisi,vyombo vya ulinzi na usalama,wadau wa uvuvi,pamoja na Wananchi wanaolizunguka ziwa hilo.
"Kwa ushirikiano huo jeshi la polisi litaweza kupata taarifa juu ya uhalifu wowote ule utakaokuwa ukifanyika katika ziwa Victoria, na nia yetu tunataka shughuli za uvuvi zifanyike bila kikwazo chochote kile kinachohusu uhalifu",alisema Sabasi
Kamishina wa polisi Liberatusi Sabasi akizungumza na waandishi wa habari Mara baada ya kufungua kikao kazi Cha kujadili hali ya uhalifu Ziwani Kanda ya ziwa
Aidha, aliwaomba wavuvi wafuate taratibu zote za uvuvi wenye tija ili kuwezesha ziwa hilo kuendelea kuwa moja ya vyanzo vikubwa vya mapato ya Serikali na mapato ya mtu mmoja mmoja.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wavuvi Tanzania (TAFU) Bakari Kadabi alisema kuwa pamoja na kuwepo kwa wizi wa mashine na nyavu katika ziwa Victoria ni lazima kikao hicho kitoe majibu ya vitu hivyo vikiibiwa vinakwenda wapi? mnunuzi ni nani? hivyo ni lazima tufatilie mlolongo wote huo ili kuweza kuhakikisha wavuvi wanakuwa salama na mali zao.
Alisema kuwa hali ya uhalifu imekuwa ikiwarudisha nyuma Sana katika kujikwamua kimaisha ndio maana wanapamba sana ili amani iweze kutawala na watu wafanye kazi ili uchimi wa Nchi uzidi kuimarika na thamani ya ziwa Victoria itazidi kuongezeka.
Mwishoooooo
No comments