Li-TAFO yaombwa kuweka utaratibu wakutoa elimu kwa viongozi wa dini
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Taasisi isiyokuwa ya kiserikali inayojihusisha na Watoto wenye changamoto ya usonji (Li-TAFO)iliyoko Jijini Mwanza imeombwa kuweka utaratibu wa kukutana na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini kwa lengo la kuwapa elimu juu ya ugonjwa huo ili wanapofika kwenye Nyumba za ibada waweze kuwaelimisha waumini wao.
Ombi hilo limetolewa na Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda wakati akifungua mbio za hisani zilizolenga kuchangia fedha kwaajili ya ujenzi wa kituo Cha kuwahudumia Watoto wenye usonji kitakacho gharimu sh milioni 500.
Pinda alisema kuwa elimu ikienea itasaidia sana watu kuondokana na fikra potofu za kuamini ugonjwa huo unatokana na ushirikina,badala yake waelewe kuwa ni ulemavu kama walivyo walemavu wengine.
Aidha, amewapongeza Rock City runners kwa namna walivyoguswa na kuaandaa mbio zenye mlengo wa kuhamasisha upatikanaji wa fedha za kujengea kituo kitakacho toa msaada kwa Watoto wenye ugonjwa wa usonji.
Kwa upande wake Shangwe Mgaya ambae ni mkurugenzi wa Li-TAFO alisema kuwa kulingana na maelezo ya wataalam Watoto wenye usonji wanavipaji Sana kwani wanauwezo wakukaliki vitu.
Watoto wakijiandaa kutoka kwenye viwanja vya Nyahingi Kata ya Mkolani Jijini Mwanza, kukimbia mbio za kilometa 3 katika mbio zilizo andaliwa na rock city runners zenye lengo la kuchangisa fedha za kujengea kituo Cha kuwahudumia wato wenye ugonjwa wa usonji
Amesema kuwa kwa Sasa taasisi hiyo inahudumia Watoto 100 lakini Kati ya hao ni Watoto 30 ndio wanaohudhuria kiliniki ya mazoezi ya viungo katika hosptali ya bugando, na hii inatokana na wengi wao kutomudu gharama za matibabu hayo kwa kukosa bima ya afya.
Mgaya aliongeza kuwa kwa Mkoa wa Mwanza bado kunaukosefu mkubwa wa wataalam wa mafunzo ya kuongea,tabia pamoja na madaktari bingwa wa mfumo wa fahamu hali inayopelekea wazazi kufuata huduma hizo katika Mikoa ya Dar -es salaam na moshi.
" Natamani Sana Mwanza tuweze kupata kituo Cha kuhudumia Watoto wenye ugonjwa wa usonji ili waweze kupatiwa matibabu, mafunzo, mazoezi ya kuongea, mazoezi ya viungo pamoja na elimu maalum",alisema Mgaya
Mwishoooooo
No comments