DC Masala: watunzeni na kuwalea Watoto katika misingi ya elimu
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala ametoa wito kwa wazazi wenye wanafunzi katika shule ya msingi Bezi kuendelea kuwatunza Watoto wao katika misingi ya elimu.
Wito huo aliutoa wakati waukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Kisiwa cha Bezi kilichopo kata ya Kayenze Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Masala alisema kuwa ni lazima tuwekeze nguvu nyingi katika elimu ili kuweza kutengeneza jamii iliyobora sanjari na hilo aliwapongeza walimu wa Shule ya msingi Bezi kwajitihada wanazozifanya za kuhakikisha Watoto wote wanajua kusoma na kuandika.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala akizungumza na Wakazi wa Kisiwa Cha Bezi kiliyochopo Kata ya Kayenze
"Nimetembelea darasa la kwanza hadi la tano Watoto wote wanajua kusoma na kuandika,endeleeni na huo moyo ili muweze kuwasaidia watimize ndoto zao,Pia mshirikiane na wazazi wao katika kuwakumbusha umuhimu wa kujisomea pindi wawapo nyumbani",alisema Masala
Aidha aliwapongeza Wananchi wa Kisiwa cha Bezi kwa namna wanavyojitoa katika kuchangia maendeleo huku akiutaka Uongozi kuwa na utaratibu wa kusoma taarifa ya mapato na matumizi kwa Wananchi hao.
"Mtendaji awe muwazi kusoma mapato na matumizi kila baada ya miezi mitatu,fedha za Serikali zinapokuja zinakuwa zimelenga kuunga mkono jitihada za Wananchi hatumuachii mtu mmoja lazima mtoe maelekezo ya pesa ilivyotumika",alisema masala
Masala aliongeza kuwa kuwa Kisiwa hicho ni miongoni mwa watu waliofanikisha ushindi wa viongozi mbalimbali katika uchaguzi hivyo yote tuliyoyaahidi kuyaleta tutahakikisha tunayatimiza kwa ufanisi mkubwa.
Mwisho aliwaelimisha na kuwahamasisha Wananchi wa Kisiwa hicho kuendelea kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa Corona kulingana na muingiliano mkubwa wa watu wanaoingia na kutoka sanjari na kupata chanjo ya UVIKO-19 kwa hiari.
Mwishoooo
No comments