Wanahabari Kanda ya ziwa Wapata mafunzo ya Sheria
Chama cha wanasheria wa Afrika masharika chini ya mkurugenzi Mtendaji Wakili David Sigano kwa kushirikiana na baraza la habari Tanzania (MCT) wameandaa mafunzo kwa waandishi wa habari, ambapo Mafunzo haya yamefanyikia jijini Mwanza.
Mwenyeji wa mafunzo haya akiwa ni Klabu ya waandishi wa Habari wa mkoa wa Mwanza (MPC) chini ya Mwenyekiti wake Ndugu Edwin Soko.
Mafunzo haya yakiwa na lengo la kuangalia changamoto na mwenendo katika suala la uhuru wa kujieleza, uhuru wa vyombo vya habari, hali ya kupata taarifa na kufanya kazi katika ufanisi kwa waandishi wa habari, sambamba na majadiliano juu ya sheria za vyombo vya habari.
Picha Mbalimbali za washiriki katika semina hiyo ya siku moja.
No comments