Breaking News

HAKIKISHENI VIKUNDI VINAPATA RUZUKU,KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge Ndg Kaspar Mmuya ametembelea vikundi vya watu wanaoishi na VVU vilivyopo chini ya Baraza la Watu wanaoishi na UKIMWI (NACOPHA) mkoani Mwanza na kujionea shughuli mbalimbali za kiuchumi zinazofanywa na vikundi hivyo.

Katika hotuba yake Katibu Mkuu Mmuya amezitaka halmashauri  zote nchini kuhakikisha zina vitambua vikundi vyote vya watu wanaoishi na VVU,Kuvisajili na kuhakikisha vinapata fedha zinazotolewa kila mwaka na halmashauri pamoja na kuvipatia ruzuku ili viweze kukua zaidi.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge Ndg Kaspar Mmuya akizungumza na viongozi wa Konga Nyamagana (Hawapo Pichani) ambapo aliwapongeza kwa kuanzisha vikundi vya WAVIU na kuwawezesha kiuchumi.


    Wanachama wa Konga Nyamagana wakifatilia hotuba ya mgeni rasimi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge Ndg Kaspar Mmuya.


   Bi Leticia Kapela Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Watu wanaoishi na UKIMWI (NACOPHA) akifatilia kwa makini mkutano wa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge Ndg Kaspar Mmuya na viongozi wa Konga Nyamagana.

 Vijana wa Konga Nyamagana wakitoa burudani mbele ya mgeni rasimi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge Ndg Kaspar Mmuya.

                                                        Na Tonny Alphonce,Mwanza.

No comments