Mamia ya wakazi wa Mwanza wavamia barabara kushuhudia mwili wa Magufuli
Ellukagha Kyusa
Mwanza
Mwili wa Hayati John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya tano umepokelewa uwanja wa ndege wa Mwanza na kuelekea uwanja wa Kirumba kwa ajili ya kuagwa na umeshuhudia mamia ya wakazi wa Mwanza wakivamia barabara ili kuona gari iliyobeba mwili ikipita.
Msafara wa kutoa mwili uwanja wa ndege wa Mwanza ulianza saa moja asubuhi huku barabara ya kutoka uwanja wa ndege kwenda uwanja wa CCM kirumba ambapo kulikuwa na wakazi wengi wa Jiji la Mwanza.
Wakazi wengi wa jiji la Mwanza walijipanga barabarani na kuangua kilio na wengine wakiwa wametandika nguo zao barabarani ikiwa ni ishara ya kuonyesha masikitiko yao ya kumpoteza mpendwa wao.
Pia msafara ulisimama kwa dakika moja kata ya Nyamanoro ambapo hayati Raisi Dkt John Magufuli aliwahi kuishi akiwa Waziri ili majirani waweze kutoa heshima zao za mwisho.
Mwili wa Dakatari Magufuli utapitishwa kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza kabla ya kuelekea Mkoa wa Geita na hatimaye Chato.
Machi 26 mwaka huu ndio siku ambayo mazishi yanataraji kufanyima kwenye Wilaya ya Chato.
No comments